Picha na
|
Picha:THINKSTOCK |
Picha na merryfarmer.net |
Picha na tvone.tv |
Ni ukweli usiojificha kuwa wanaume wamekuwa
mstari wa mbele kuchukua majukumu mbali mbali ya familia yahusuyo kutoa
pesa.Ingawaje katika kipindi hiki cha mabadiliko ya kiuchumi na teknolojia
tunaona pia wanawake wakichukua nafasi kubwa ya kubeba majumu ya familia
yahusuyo kutoa pesa.
Najua kila mtu atakuwa na mtazamo tofauti
kuhusiana na swali letu la leo.
Nikitumia uzoefu wangu wa kutazama kwa
ukaribu masuala ya familia…chukua mfano umeenda sehemu ya starehe(hotelini),
chunguza kwa makini, nani analipa bili ya mapochopocho yaliyoliwa na vinywaji?
Ni mwanamke au mwanaume? Jibu unalo!
Kautaratibu haka huendelea kujijenga kuanzia
kipindi cha uchumba hadi wakati wa ndoa.
Tatizo linakuja pale wanandoa wanapokuwa wote
wana kipato…utaona utata, mume huanza kumbadilisha mwanamke ghafla kwa
kumwambia aanze kutoa pesa kwa matumizi mbali mbali ya nyumbani.Jibu la mke
huwa ”wewe ndiyo baba na kichwa cha familia…hivyo una wajibu wa kubeba majukumu
yote.” Ndiyo hivyo, hakuzoea kulipia bili tangu kipindi cha uchumba…anajua
kuwa mwanaume ana jukumu la kulipia gharama zote za familia.
Hapa ndipo ugomvi unapoanzia kuhusiana na
mapato na matumizi ya pesa kwa kila mmoja.
Utaratibu huo unaweza kubadilika, hasa
ikizingatiwa kuwa mahusiano na ndoa ni makubaliano wa mwanaume na mwanamke
yakilenga kusaidiana na kujenga familia iliyo imara.
Tunaanzia wapi sasa kubadilisha mfumo?
1. Mwanaume
una jukumu la kumzoesha mwanamke wako kuanza kulipa au kuchangia bili au
gharama nyingine za matumizi (haijalishi kama wewe mwanume unampa pesa)
…inapaswa aonekane analipa au kuchangia...
2. Mwanamke,
huna sababu ya kukubali kulipiwa mara kwa mara…onyesha kuwa nawe
una uwezo wa
kulipa au kuchangia, hivyo huwezi kutetereshwa na hutanyanyasika wala kufanywa
mtumwa wa mwanaume.
3. Lifanye
zoezi lenu kuwa endelevu na mtaona mtunda yake.Hapa ndipo lile lengo tarajiwa
la kusaidiana kwenye ndoa linapojidhihirisha.Pia kuepusha ugomvi unaohusiana na
matumizi ya pesa kwa kila mmoja.
Picha na myhappyfinds.com |
Anzia hapo kubadilisha mtazamo ili kuepusha migogoro ndani ya familia!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!