M
|
akala hii ni
muendelezo wa makala ya Jumapili, 27 Octoba 2013 katika eneo la elimu kuhusu
mtazamo wa Kisaikolojia kuhusu adhabu ya viboko mashuleni:
Picha www.brisbanetimes.com.au |
1.CHUNGUZA CHANZO CHA TABIA MBAYA YA MTOTO
Hupaswi kumwadhibu mtoto/mwanafunzi kwa viboko au adhabu
nyingine ya kuutesa mwili wake kama amekiuka kanuni, au kuonyesha tabia mbaya.
Fuatilia kwa makini ukitafuta chanzo cha mabadiliko ya tabia
yake,mpatie ushauri nasaha ukimfanya ajichunguze tabia yake, wakati huo huo ukimuelekeza
madhara ya tabia yake mbaya.
Kubaliana naye kubadilika kwa kupanga naye mikakati iliyo na
faida kwa mtoto/mwanafunzi(mfano-mkakati utakao chochea kujisomea na kuepuka
tabia mbaya.
2. KEMEA TABIA MBAYA
Onyo litolewalo kwa mdomo ni adhabu yenye kugusa hisia ya
ndani kwa mtoto/mwanafunzi kuliko adhabu ya viboko.Kemea kuonyesha
kutoridhishwa na tabia mbaya au ufunjivu wa kanuni na maadili.
Zingatia: Mbinu hii ni nzuri na ina matokeo mazuri
kama tu haitatumika mara kwa mara.Mtoto/mwanafunzi huweza kuchukulia kama
mazoea na kutoa tafsiri kuwa mwalimu/mzazi ana hasira/mkali wakati wote
ikitumika mara kwa mara.
3. TAFAKARI KWA PAMOJA NA MTOTO/MWANAFUNZI KUHUSU TABIA MBAYA
Tenga muda wa kukaa na mtoto/mwanafunzi kujadili madhara ya
tabia mbaya au kukiuka kanuni mlizokubaliana.
4. TUMIA ZAWADI KUCHOCHEA TABIA NJEMA
Pongezi kwa mtoto/mwanafunzi huchochea kuendelea kwa tabia
njema.Inaweza kuwa ya kitu cha kushikika au maneno ya pongezi.
Pia, mpongeze mtoto/mwanafunzi anapoonyesha kuwa na tabia
njema.
Angalizo:Unapaswa kuwa makini sana katika
kutoa zawadi kwa mtoto/mwanafunzi.Anaweza
kuigiza tabia njema ili akufurahishe ilihali amaanishi kutoka moyoni. Ni vizuri
kutompa mtoto/mwanafunzi zawadi mara kwa mara kila anapokufurahisha/anapoonyesha
tabia njema.Kufanya hivyo hupoteza maana halisi ya zawadi, mwisho
mtoto/mwanafunzi huchukulia zawadi kama mazoea au kitu cha lazima akiwa ameonyesha tabia njema.
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni