Nakuletea
makala hii fupi ikiwa ni sehemu tu ya yale yaliyojili siku ya wiki ya
maadhimisho ya kuzaliwa shujaa wa Afrika-Nelson Mandela “Madiba” kuanzia
Julai,12-18,2014 katika Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia-Tengeru,Arusha.
Kwa
wiki nzima kulikuwepo na maonyesho ya ubunifu wa Kisayansi na elimu za hadhara
zikijumuisha wataalam mbali mbali wa Sayansi na Teknolojia kutoka vyuo vya hapa
nchini na nje ya nchi.
Nikiwa
mwanachuo, nilitembea mabanda mbali mbali ya kibunifu.Nilivutika na ubunifu wa
mtaalamu, mjasiriamali Bw. Justin Mungure wa Makumira, Arusha kwa ubunifu wake wa
kuibadilisha TOYO ya magurudumu matatu maarufu kwa kubeba mizigo kuwa ya
magurudumu manne muonekano kama ule wa gari.
Picha:Muonekano wa pikipiki aina ya TOYO ya magurudumu matatu. |
Niliweza kumhoji mtaalamu, ilikuwaje kufikia ubunifu wake? Alijibu; “mara nyingi nimeona TOYO za magurudumu matatu zikianguka kwa kukosa nguvu ya mbele ya gurudumu moja…hivyo nikaamua kuiboresha zaidi kwa kuifanya iwe na magurudumu mawili sawa na nyuma…na sijabadilisha mfumo mwingine wa mashine…”
Picha:TOYO ya magurudumu manne-Ubunifu wa Justin Mungure. |
Mungure anifanya kazi hiyo katika karakana yake iliyopo eneo la Makumira-Jijini Arusha.Hubadilisha TOYO ya magurudumu matatu kwa gharama ya takribani shilingi milioni moja na nusu za kitanzania(1,500,000/=) licha ya gharama ya kununua TOYO mpya.
Nilihamasika sana na
ubunifu wake ndiyo maana nimependa kukushirikisha ndugu msomaji kuwa tunaweza
kubadili mtazamo wa kufikiri na kuamini katika masuala mengi katika maisha yetu
ikiwemo jinsi ya muonekano wa vitu mbali mbali na hata yale yahusuyo Teknolojia
kwa lengo la
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza! Social Enterprise.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni