Makala inayofanana: NJIA TANO (5) ZA KUWAFANYA WATU WENGINE WAKUAMINI KWA NIA NJEMA KABISA.
Ndugu msomaji na mfuatiliaji
wa Jielimishe Kwanza Blog, unapaswa
kujua kuwa kuna watu au makundi ya watu hapa duniani hutumia njia za ujanja
ujanja na pia kuchanganya na saikolojia ya maisha ya binadamu ili
kujinufaisha.Hutumia ujanja huo kuwaaminisha wengine wanachoamini na mwisho wa
siku hutumia migongo na ufikiri hafifu wa wengine kujineemesha.
Bila kificho nakuletea viashiria
VITANO (5) ili kukuweka wazi ndugu msomaji na ujue kuwa katika viashiria hivyo
vinavyoainishwa unataka kutumika au unatumika kwa maslahi ya wengine.
1.SIKU ZOTE HUONYESHA KUWA NA MAMLAKA
Katika kila mahojiano na
majadiliano yenu huonyesha kuwa ni wenyewe pekee wanaoweza kutatua tatizo
husika kwa wakati husika. Hivyo kukufanya uwe mtu wa kusindikiza mawazo na
matakwa yao.
2.WANAAMINI SANA MAWAZO YAO NA KUBEZA YA
WENGINE…
Kiashiria hiki hakina
tofauti sana na namba 1, tofauti ni
kuwa wao hupenda kupuuza na kubeza mawazo ya wengine wazi wazi kwa makusudi na
baadaye huyatumia yale ya msingi kwao kwa manufaa binafsi.
Ni watu walio mafundi wa
kukatisha tamaa kwa kutumia maneno yenye uzito katika hali iliyo halisi.Hutumia
takwimu kwa namba halisi na nukuu mbali mbali kubeza mawazo ya wengine.
3.WANAJIAMINI SANA KWA YALE WANAYOYASEMA
BILA KUBADILIKA BADILIKA
Kujiamini ni silaha yao
kubwa.Wanaelewa maana halisi ya kujiamini kwa kile wanachoeleza na ni rahisi
kwao kukuaminisha wanachoamini kwa matakwa binafsi.
4.HUJENGA HOJA NZITO KUPITIA HOJA YAKO
Huunganisha kiashiria hiki na kiashiria namba 2; kubeza mawazo yako lakini kwa
upande mwingine hutumia hoja yako kutoa hoja nzito iliyo na maslahi kwao.
5.HUONYESHA MAPUNGUFU YA KATIKA HOJA ZAKO
Ni mahili sana wa kuchunguza
na kuelezea mapungufu ya wengine katika lugha ambayo utaridhika.Mwisho wa siku
hutumia mapungufu yako na kuyaboresha kwa manufaa yao binafsi bila hata
kukushirikisha.
_________
Ndugu msomaji wa makala hii
usifikiri watu hao ni “magenius” au
wana uwezo wa kipekee kwa kupendelewa na Mungu; La hasha! Ni wepesi tu wa kujifunza, kujielimisha kwanza na kusoma
vitabu mbali mbali vilivyosheheni maafunzo na uzoefu wa maisha ya watu
waliofanikiwa kwa kupitia saikolojia ya maisha ya binadamu.
Kazi kwako, je unataka
kuendelea kutumika na hao wajanja kwa maslahi zao binafsi au unachukua hatua
ya ujasiri kubadilika na kuhama hapo ulipo kifikra na kimtazamo? Jibu unalo!
Makala hii imeandaliwa kwa kutumia ubunifu na uelewa
binafsi wa kisaikolojia wa mwandishi Henry Kazula kwa kushirikiana na vitabu mbali mbali vya kisaikolojia.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza
Ni kweli Henry!
JibuFutaHapo naona umehamasisha kusoma vitabu na kujifunza
JibuFuta