Katika kipindi hiki cha utandawazi na
uwepo wa soko huria nchini Tanzania kumeibuka wimbi kubwa la watu kupenda kuanzisha na kumiliki biashara
binafsi au katika vikundi ili kupambana na tatizo la ajira nchini.
Kwa bahati mbaya, wafanyabishara walio wengi
wamekuwa wakiangukia katika biashara ndogo ndogo na zisizo katika mfumo rasmi,
pia hazitambuliki kisheria kwa hofu ya kuhitaki mitaji mikubwa ndipo wasajiliwe; hivyo, kukosa wigo mpana wa kukuza biashara
zao na kukosa fursa kem kem za kupata zabuni za Serikalini au kushirikiana na
wafanyabiashara wakubwa walio katika mfumo rasmi unaotambulika kisheria.Pia
kushindwa kupata urafiki wa karibu na Sekta zinazohusika na kusaidia
wajasiriamali wadogo kupata fedha kukuza biashara zao.Hizo ni baadhi ya
hasara za kushindwa kusajili Kampuni au Jina
la Biashara yako na kutambulika kisheria.
Baada ya kuiona changamoto iliyopo kwa
wafanyabishara/ wajasiriamali wadogo wenye nia ya kukuza wigo wa biashara hata Kimataifa, Kampuni
ya Jielimishe Kwanza imefanya utafiti wa kina, pia kupitia Mamlaka inayohusika nchini Tanzania
na kukuainishia njia rahisi za kufuata ili utoke hapo ulipo na kuifanya kampuni
yako itambulike kisheria na kukua, pia kuongeza wigo wa biashara yako.Tambua kuwa kampuni zisizo na malengo ya
kukua kwa kuongeza ubunifu zipo kwenye hatari kubwa ya kupotea katika ramani ya
biashara ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa biashara.
Je, bado unasitasita kuwa na kampuni
binafsi kisheria? Hujachelewa, haijalishi una mtaji mdogo, ikiwa inaitwa
biashara yenye kuleta kipato halali ni vizuri kuisajili kisheria. Hivi sasa
mfumo wa usajili umerahisishwa sana; sasa unaweza kusajili jina la Biashara na Kampuni
yako kwa njia ya mtandao wa Internet (Business Name Online Registration),
weka mpango mkakati kuanza kujisajili na kufuata yafuatayo;
- Utalazimika kuingia kwenye internet katika mtandao wa http://www.brela.go.tz/
- Jisajili* (SIGN UP) katika mfumo huo wa mtandao (ikiwa unasajili kwa mara ya kwanza); INDIVIDUAL ikiwa ni akaunti binafsi na CORPORATE kwa kampuni iliyokwisha sajiliwa.* Ili uweze kusajili unapaswa kuwa na vitu vifuatavyo i) Email ii) Nambari ya simu iii) Nambari ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya biashara au hati ya kusafiria.Ukimaliza kuingiza taarifa zako, mfumo wa usajili utatuma Nenosiri (Password) kwenye email yako.Hivyo, utatumia Email yako na Nenosiri kuingia kwenye mfumo rasmi ya usajili.
Hakikisha
una majina matatu (3) pendekezwa ya Kampuni yako. Ukiwa umefuata hatua zote; ( hatua
ya 1 na 2), bonyeza BUSINESS NAME CLEARENCE (kwa
usajili wa jina la Biashara, ambao unaishia online) na COMPANY NAME CLEARENCE (kwa usajili wa jina la Kampuni), kisha APPLY
NEW COMPANY NAME ingiza jina la Kampuni unalotaka kusearch kisha SUBMIT, hapo
utakuwa umeomba jina baada ya Mamlaka husika kufanya search.Ikiwa jina
limekataliwa (REJECTED) utatakiwa kufuata maoni elekezi au kuomba jina lingine
kwa kubonyeza APPLY NEW COMPANY NAME, na kama jina likiwa limekubaliwa APPROVED
READ TO REGISTER hapo utatakiwa kulipia jina hilo kwa mfumo rasmi ambao mfumo
utaelekeza na hivyo kuandaa MEMORANDUM and ARTICLES OF ASSOCIATION na kujaza
FORM NO 14A na 14B kisha ziwasilishwe kwenye ofisi ya Mamlaka husika ya
usajili kwa kufanyiwa tathmini ili ulipie ada ya usajili kulingana na thamani
ya Kampuni yako. Fahamu zaidi kuhusu Ada ya usajili wa
Kampuni na usajili wa Jina la
Biashara.
Mwisho baada ya kufanikiwa kusajili,
utapatiwa cheti cha usajili.Baada ya hapo utahitajika kughulikia kupata namba
ya mlipa kodi (TIN) ambayo hutolewa BURE kupitia TRA na leseni ya biashara
kutoka Manispaa ambayo biashara yako ipo.
Ikiwa unahitaji usaidizi zaidi au upo
nje ya Dar es salaam unaweza kuwasiliana nasi;
Simu: +255 754 572 143 / +255 716 075 826
E-mail: jielimishekwanza@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni