Jumatano,1 Mei 2013
Wafanyakazi nchini wanaungana na wafanyakazi wote duniani kuadhimisha siku hii muhimu kwao.Sherehe ya kilele cha siku hii kinafanyika jijini Mbeya huku mgeni rasmi akiwa raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Dr.Jakaya Mrisho Kikwete.
____________________
__________________________________________
Itafahamika
kuwa wafanyakazi katika sekta zote wanayo ya moyoni kuweza kumpatia
mheshimiwa raisi.Kubwa kuliko lote ni maslahi duni isiyoendana na
mabadiliko ya uchumi na maendeleo ya nchi.
Katika kipindi kirefu kumekuwa na migogoro ya hapa na pale hasa katika sekta ya madaktari na walimu.Athari za migogoro hiyo imejionyesha wazi huku wananchi wakieleza lawama kwa serikali sikivu.
Katika kipindi kirefu kumekuwa na migogoro ya hapa na pale hasa katika sekta ya madaktari na walimu.Athari za migogoro hiyo imejionyesha wazi huku wananchi wakieleza lawama kwa serikali sikivu.
Nategemea,
mwishoni wa sherehe hii kutakuwa na suluhisho la migogoro hiyo,lengo ni
kuboresha hali ya utendaji katika sekta mbali mbalimbali nchini.
Ndugu zangu wasomaji, nitajitahidi
kuiwasilisha hotuba kuu kutoka kwa mheshimiwa raisi ili tuelewe msimamo
wa serikali kwa wafanyakazi nchini hasa katika mwaka ujao wa fedha...
Je, mshahara unaoupata unalingana na umuhimu wako kazini?
Ijumaa,19 Aprili 2013-Saa 7.00mchana
Kwa
kipindi kirefu nimekuwa nikifuatilia matatizo ya migogoro ya
Wafanyakazi na Serikali kuhusu mishahara midogo.
Nikajaribu kufuatilia kwa kina, hivi kwa nini kuna utofauti mkubwa wa ngazi za mishahara kwa kada mbalimbali? Nikakutana na muongozo ufuatao kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, imeeleza kuhusu haki ya kufanya kazi
22. -(1) Kila Mtu anayo haki ya kufanya kazi.
23. -(1) Kila Mtu, bila ya kuwapo ubaguzi wa aina yoyote, anayo haki ya kupata ujira unaolingana na kazi yake, na watu wote wanaofanya kazi kulingana na uwezo wao watapata malipo kulingana na kiasi na sifa za kazi wanazozifanya.
Bila shaka utakuwa umepata jibu ni kwa nini unapata kiwango hicho cha mshahara. Naomba ujiulize maswali yafuatayo ili uanzie hapo ulipo;
- Je, unajituma kazini ili kuongeza uthamani wako kazini?
- Je, unajituma kwa mwajiri wako zaidi kuliko unavyojituma mwenyewe?
- Je, umejiwekea mikakati gani ya kujiongezea ujuzi katika fani uliyonayo ili kuongeza thamani yako kwenye soko la ajira?
- Je, una ujuzi wa kutosha kuweza kutimiza majukumu ya kazi yako?
- Je, uwepo wako kazini unamletea faida mwajiri wako au faida kwako mwenyewe?
- Je, umejipangaje kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia kwa karne hii ya 21?
Unaweza
kujisomea makala yangu kuhusiana na nini ufanye ili kupambana na suala
la mishahara na si kubeba mabango barabarani na kupambana na polisi.
Fuatilia:Modern-Day Slavery by Henry Kazula
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni