Jumamosi,11 Mei 2013
Kuna viumbe ambao ni adimu sana, mfano faru,Hii ni kutokana na hali yao ya kuzaliana; kuna mpishano mkubwa wa miaka ya kuzaliwa kati ya mmoja na mwingine.Pia huzaa idadi ndogo ya vizalia.Viumbe hawa adimu wanapaswa kutunzwa kama mboni ya jicho kwa mantiki kwamba wapo kwenye hatari kubwa ya kutoweka duniani.
Jumapili, 28 Aprili 2013 7.17usiku
Utafiti uliofanywa na wanasayansi katika maabara ya serikali nchini Marekani huko Hawaii zimethibitisha kuwepo kwa ongezeko kubwa zaidi la hewa ukaa duniani kufikia mia nne kwa milioni moja ya sehemu za dunia. Ongezeko hili ni la kwanza kihistoria.
Wakiripoti kupitia BBC Swahili, walieleza kuwa ongezeko hilo liliwahi kutokea miaka milioni tatu hadi milioni tano iliyopita ambapo ilikuwa chini ya mia nne kwa sehemu milioni moja za dunia(400ppm).
Wanasayansi hao wamebaini kuwa kuna sababu mbali mbali zinazochangia ongezeko la hewa ukaa duniani, hasa ni hewa ukaa itokanayo na gesi inayotengenezwa na binadamu.
Hii ikimaanisha kuwa ongezeko kubwa la idadi ya watu limepelekea ongezeko kubwa la hewa ukaa.
Vile vile, walibaini kuwa ongezeko kubwa la hewa ukaa limepelekea kuongezeka kwa joto duniani mara dufu.
__________________
Gesi kutoka viwandani katika kuchangia ongezeko la hewa ukaa. www.rose-kajivo.blogspot.com |
Nikiungana na sababu moja ya kuwa binadamu ndiye chanzo cha ongezeko la hewa ukaa duniani na nyingine ambazo hazikuanishwa, naweza kusema kubwa ni shughuli za binadamu hasa ongezeko la viwanda duniani vinavyotoa hewa ukaa kwa wingi, utumiaji wa magari na motokaa hasa yale mabovu.
Sababu nyingine ni uharibifu mkubwa wa misitu ambayo kisayansi ina mchango mkubwa sana katika kupunguza hewa ukaa kupitia mfumo wa utengenezaji wa chakula.
Uharibifu wa mazingira unachangiwa sana na umasikini uliokithiri hasa katika nchi za Afrika.Pia kubadilisha maeneo la misitu kuwa makazi ya kudumu.
Kukata miti kama kuni kwa matumizi ya nishati www.lukwangule.blogspot.com |
Juhudi za makusudi zinapaswa kuchukuliwa na hasa zinaanza na usimamiwaji mzuri wa sera na sheria na kanuni za kila nchi kuhusu utunzaji wa mazingira.
Ukiangalia kwa kina kuhusu chanzo cha tatizo, kinahusu nchi zilizoendelea(kupitia viwanda vikubwa na utumiaji wa magari na motokaa) na nchi zinazoendelea (ukataji wa miti kwa matumizi ya nyumbani kama nishati ya kupikia, magari mabovu na yenye kiwango cha chini).
Tunaweza pia, kuanzia hapo, hasa kwa kubadilisha gesi za viwandani kwa matumizi mengine na si kutupiwa angani.Kupunguza matumizi ya motokaa na magari binafsi hasa yale mabovu na yaliyo chini ya kiwango.
Tunaweza kupunguza matumizi ya magari
|
Tuhamasishe upandwaji wa miti kila mahali panapostahili na kuzuia ukatwaji wa miti usikuwa na tija.Ni vyema kuyaboresha maeneo kama mashimo yaliachwa kwa shughuli mbali mbali kuwa misitu.
Tukumbuke kuwa, mabadiliko ya kuifanya dunia yetu kuwa sehemu nzuri ya kuishi yanaanza na mtu mmoja.
Na Henry Kazula.
Jielimishe Kwanza! Chukua hatua...
Jukumu letu kuwatunza na kuwahifadhi viumbe hawa adimu...
Jumapili, 28 Aprili 2013Kuna viumbe ambao ni adimu sana, mfano faru,Hii ni kutokana na hali yao ya kuzaliana; kuna mpishano mkubwa wa miaka ya kuzaliwa kati ya mmoja na mwingine.Pia huzaa idadi ndogo ya vizalia.Viumbe hawa adimu wanapaswa kutunzwa kama mboni ya jicho kwa mantiki kwamba wapo kwenye hatari kubwa ya kutoweka duniani.
Inafahamika
kwamba viumbe vyote duniani huishi kwa kutegemeana na endapo kutatokea
upungufu au kutokuwepo kwa kiumbe fulani, hupelekea kuharibika kwa
mlishano ulio sahihi kwenye eneo husika viumbe vinapopatikana.
Ni
jukumu letu kuwatunza viumbe hao adimu na ikiwezekana kuwazalisha
katika maeneo mengi duniani kuzingatia na mazingira furahishi kwa viumbe
hao.
Taarifa nyingine:
http://www.slideshow.com/users/heka/extinction-of-species-690254261
http://mazingira-leat.blogspot.com/2010/10/vyura-wa-kihansi-thamani-ya-maliasili.html
Taarifa nyingine:
http://www.slideshow.com/users/heka/extinction-of-species-690254261
http://mazingira-leat.blogspot.com/2010/10/vyura-wa-kihansi-thamani-ya-maliasili.html
Suala la koboresha mazingira linaanza mtu mmoja...hivyo usidharau jitihadaya mmoja!
Jumapili, 28 Aprili 2013 7.17usiku
Leo
katika mazingira tunakutana na raia wa India alivyoweza kuonyesha uwezo
wake na dhamira ya dhati ya kujali mazingira.
Amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupanda miti kwenye eneo la hekali 1,360 kwa mikono yake katika kipindi cha miaka 30. Kweli usije dharau nguvu ya "mmoja"- Never underestimate the power of "one".
Amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kupanda miti kwenye eneo la hekali 1,360 kwa mikono yake katika kipindi cha miaka 30. Kweli usije dharau nguvu ya "mmoja"- Never underestimate the power of "one".
Hii iwe changamoto kwa kila mtu kujali mazingira.Hapa ananikumbusha maneno ya Mahtma Gandhi kuwa
“Be the change that you wish to see most in your
world”-Tuwe chanzo cha mabadiliko tuyatakayo katika maisha yetu.
Suala la mazingira ni nyeti sana, linagusa maisha ya kila kiumbe, ikiwa binadamu ndiye anayeongoza kwa uhalibifu wa mazingira hiyo kutovitendea haki viumbe vingine.
Suala la mazingira ni nyeti sana, linagusa maisha ya kila kiumbe, ikiwa binadamu ndiye anayeongoza kwa uhalibifu wa mazingira hiyo kutovitendea haki viumbe vingine.
Kama
kila mmoja atasimama kuchukua hatua za makusudi kuyalinda mazingira
tutaepukana na majanga mbali mbali yanayoambatana na uharibifu wa
mazingira...
Habari zaidi: http://www.mnn.com/earth-matters/wilderness-resources/stories/indian-man-single-handedly-plants-a-1360-acre-fores
Hi! Would you mind if I share your blog with my myspace group?
JibuFutaThere's a lot of people that I think would really enjoy your content. Please let me know. Thanks
Check out my web-site; laser cellulite treatment