www.syracuse.com |
Watoto wengi wanaamini na kuheshimu maagizo yatolewayo kutoka katika vipindi mbali mbali, hivyo kupingana vikali na maagizo/matakwa ya wazazi/walezi.
Hapa utagundua kuwa muongozo wa tabia za watoto wetu unategemea na kuathiriwa sana na kupishana kwa itikadi mbili tofauti; yaani zile za kwenye vipindi visivyo na tija kwenye televisheni na zile za wazazi/walezi.
Tatizo hili limewapelekea watoto wengi kukosa maadili na kushuka kwa
taaluma zao na kushindwa kuwa na muda wa kujipangia malengo yao ya
baadaye, hivyo kutengeneza kizazi kisichojitambua, kisichokuwa na
malengo wala muelekeo.Yaani ni kizazi cha bendera fuata upepo.
Pia kuna matatizo mbali mbali ya kiafya kwa mtoto yatokanayo na kukaa muda mrefu kwenye televisheni au intaneti, nayo ni;
www.mirror.co.uk |
- Kuongezeka uzito isivyo kawaida
- Maumivu ya macho kutokana na mionzi
- Kuumwa kichwa
- Ubongo kushindwa kuimarika hasa kwa watoto walio chini ya miaka 2
- Kuwa kwenye hatari ya kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya...
Kutokana na utafiti nilioufanya kwa kushirikiana na tafiti nyingine, nimegundua mbinu zifuatazo ambazo wewe
kama mzazi/mlezi ukizisimamia kikamilifu zitamsaidia mtoto wako, nawe kuishi maisha
ya furaha pamoja na familia yako:
1.Mfanye mtoto wako kuwa msomaji wa vitabu, wewe ukiwa mfano
Mzazi/mlezi unatakiwa kusoma vitabu mbali mbali na pia kumsomea mtoto kitabu na kutoa simulizi mbalimbali kutoka kwenye vitabu.Mpatie majukumu ya kufanya kutoka katika vitabu alivyosoma; hasa kuandika taarifa fupi ihusuyo kitabu husika.
2.Mfanye mtoto aweze kuchagua vipindi vya kuangalia,wewe ukiwa mfano
Inatakiwa
ieleweke kuwa, si kila kinachoonekana kwenye Televisheni kinafaa
kuangaliwa na kila mtu.Makampuni mengi huandaa vipindi kwa lengo la
kufanya biashara na kwa kiasi kidogo kuelimisha umma.Mzazi/Mlezi
unatakiwa kuwa mfano wa kuigwa katika suala hili na si kuwa mtu wa
kuruhusu uozo wa aina yoyote ile.Anza kumkuza mtoto kwa maadili mema na
atakulia katika njia hiyo.
3.Panga utaratibu unaoeleweka kwa kila mwanafamilia
Kuishi
maisha yasiyo na mpangilio ni hatari kubwa. Ni vizuri kuwa na utaratibu
mzuri wa kula, kusoma, na kulala.Ni dhahiri kuwa wazazi/walezi mna
majukumu mengi, lakini yasiwafanye kuepuka na kuwa kisingizio cha
kutotimiza wajibu wenu.
4.Toa zawadi kwa mtoto akipunguza muda wa kuangalia televisheni
Inaweza
kuwa ni zawadi inayohusisha matembezi ya kawaida au kutembelea
matamasha, pia unaweza kumpatia mtoto zawadi ya nguo, vitabu au CDs
zenye mafunzo. Hii itamfanya mtoto kupata msukumo zaidi wa kupunguza
muda wa kukaa kwenye televisheni.
5.Fanya utaratibu wa matembezi kwenye vivutio mbalimbali
6.Usiweke televisheni kwenye chumba cha watoto
7. Mjengee mtoto kuwa kujifunza kunawezekana kwa kuona hali halisi na si lazima televisheni
Mzazi/Mlezi unaweza kutumia vitu asilia katika mazingira yanayotuzunguka kumssaidia mtoto kujifunza na si kutegemea afundishwe na Televisheni na intaneti.
8.Mweleze mtoto hasara za kutumia muda mwingi kwenye televisheni na intaneti
9.Mhusishe mtoto kwenye klabu za michezo na vikundi vya sanaa ili kukuza kipaji chake
10.Weka namba ya siri kwenye televisheni na kuiwasha pale inapohitajika
11.Hakikisha unakuwa na muda wa kujumuika na familia yako
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni