UTUMIAJI WA MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA:
Jumanne, 14 Mei 2013
Madhara ya matumizi ya madawa haya yapo
wazi, kila kijana na jamii kwa ujumla anayaona kutoka kwa wengine waliotumia awali...
Pia kuna kundi jingine la vijana wanatumika kubeba na kuyauza madawa hayo hatari.
Biashara hii hatari huweza kuwa kishawishi kikubwa cha kuyatumia madawa hayo na kuhatarisha afya zao.
Hii hali si njema kwa mwelekeo wa Taifa letu.Hatari kubwa ni kupungua kwa nguvu kazi ya Taifa.
Karibu utoe maoni yako...
Imetolewa na Jielimishe Kwanza!
Jumanne, 14 Mei 2013
www.docbig.com |
zangocweb.org |
www.tkd.motivplus.hr |
Kwa
kipindi kirefu sana nchini Tanzania kumekuwa na taarifa kuwa vijana
wengi wamejiingiza katika mkumbo wa kutumia madawa ya kulevya kama vile
bhangi,mirungi, na mengineyo.
Vijana wengi wamekuwa wakiyatumia madawa hayo kwa kuwa
na fikra mbalimbali, hasa wengi wakisema na kuamini madawa hayo yanawaburudisha na
kuwafanya wasahau matatizo yao kama ukosefu wa ajira na maisha magumu.
Wengine wanajikuta wakifuata mkumbo wa makundi ili wakubalike kwenye kikundi.
Pia kuna kundi jingine la vijana wanatumika kubeba na kuyauza madawa hayo hatari.
Biashara hii hatari huweza kuwa kishawishi kikubwa cha kuyatumia madawa hayo na kuhatarisha afya zao.
Hii hali si njema kwa mwelekeo wa Taifa letu.Hatari kubwa ni kupungua kwa nguvu kazi ya Taifa.
Je,
unafikiri nini kinasababisha vijana wengi kuendelea na matumizi ya
madawa haya hatari ilihali wanajua fika madhara yake? au wengine bado
hawajui madhara ya madawa hayo?
Imetolewa na Jielimishe Kwanza!
kwanza hili ni janga la taifa zima kiukweli maisha yetu ka vijana yanaendesha na mihemko na mkumbo. Sijui vijana tunawazaga nini kuhusu haya madawa ya kulevya mi ningependa vijana tujikusanye makundi labda hili tatizo la ajira lisiwe kisingizio basi tunashindwa hata kutengeneza viwanda vidogo vidogo. Pili vijana wengi wabinafsi wanajiangalia wao kwanza wanataka wanufaike wakiwa wao wenyewe umoja siku zote ni nguvu
JibuFuta