Jumatatu, 13 Mei 2013
Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwa ushirikiano na Kitivo cha Ujasiriamali cha Chuo kikuu
Picha na Henry Kazula-Mshiriki wa mafunzo |
cha Dar-es -salaam (UDEC) wamefanikiwa kuanzisha mafunzo kwa wahitimu na wajasiriamali wanao chipukia wa vyuo vikuu leo katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Katibu Mtendaji wa Dkt. Annacleti Kashuliza akifungua mafunzo hayo ya wiki 3 kwa Vijana 40
waliohitimu shahada mbali mbali katika vyuo vikuu tofauti nchini, ameeleza changamoto mbali mbali Taifa ilizonazo kuhusiana na ukosefu wa ajira kwa vijana.
Aliianisha kuwa ajira ni chache, hivyo ni vyema vijana wakawezeshwa kujiajiri, pia kuweza kuajiri vijana wengine.
Hata hivyo, Dkt. Annacleti Kashuliza alitoa sababu mbali mbali zinazopelekea vijana wengi kushindwa kujiajiri; moja ni ukosefu wa mbinu za kuendesha biashara, kukosa mitaji, kukosa taarifa sahihi kuhusu biashara na kushindwa kupata mitandao ya kusonga mbele kibiashara.
Hivyo basi, mafunzo hayo yaliyoanza leo tarehe 13 Mei 2013 hadi 31 Mei 2013 yanalenga kuwajengea vijana uwezo katika miraji waliyoianza na pia kuweza kuboresha mawazo mbali mbali ya miradi ya biashara tarajiwa.
Sambamba na mafunzo hayo vijana watapata fursa ya kuonana na kuongea na wajasiriamali vijana waliofanikiwa ili kushirikishwa uzoefu.Pia kuunganishwa na mitandao mbali mbali ya kupata mikopo.
Imeandikwa na Henry Kazula.
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni