Picha na hot100tips.com |
Mara
kwa mara watu wamekuwa na manung’uniko yaliyo sanjali na hali ngumu ya
maisha.Hii imewafanya wengi kukosa muelekeo na mwishowe kukata tamaa, hasa
waonapo wengine wakitesa na maisha.
Watu wamesongwa na kulaumu huku wakitumia
muda mwingi kusononeka bila kuchukua hatua ya kufikiri tofauti.Ijulikane kuwa
jinsi utumiavyo muda mrefu kusononeka na kunung’unika ndivyo unavyojiweka
kwenye nafasi kubwa ya kupoteza fursa nyeti za kukutoa kimaisha.
Yafuatayo ni baadhi tu ya madhara ya kuwa na mtazamo hasi
wa maisha;
- Utajiona huwezi kila kitu
- Utakuwa msindikizaji wa maamuzi ya watu, hutaamini maamuzi yako
- Utatofautiana na watu wenye mafanikio kifedha mfano; utachulia watu wote wenye fedha ni wezi ,mafisadi, na washirikina.
Mwandishi
maarufu, mfanyabiashara mkubwa nchini Marekani – Robert Kiyosaki
aliwahi
kusema;
“what you think it’s real, becomes
your reality” kwa lugha ya Kiswahili- “unachofikiri ni halisi kinakuwa uhalisia wako”akitoa mfano kuwa mtu akisema siwezi kuwa tajiri, mtazamo huu huwa halisi kwake
kwa sababu hatakuwa na juhudi zozote za kumpeleka hatua ya kuwa tajiri.
- Utapoteza fursa nyingi za kukutoa kimaisha
- Kukosa ujasiri na uthubutu wenye tija mfano mtu anaweza kusema “nikijaribu kufanya biashara hii nitapata hasara…anaweka uhakika wa kupata hasara kabla ya kuanza biashara yenyewe, hivyo kutothubutu.
Wakati mwingine nitajitahidi kukuletea mbinu
za kuwa na matazamo chanya. “JIFUNZE KUWA NA MTAZAMO CHANYA.” Ukitumia mbinu
hizo zitakubadilisha sana, hutakuwa kama ulivyokuwa.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni