Malezi
bora ya watoto huchangiwa na ushirikiano wa pamoja wa baba na
mama.Kisaikolojia, mtoto hujengeka na kuwa na furaha kutokana na kuwepo kwa
furaha na upendo wa wazazi.
Ifahamike
kuwa muunganiko wa wazazi kwa ndoa au la unaimarika zaidi kwa kuwepo na
mtoto/watoto. Licha ya kuwepo na tofauti za hapa na pale ndani ya wapendanao
lakini haitakiwi watoto wajue tofauti zilizopo.
Picha imetolewa:www.ehow.com |
Ugomvi
wa aina yoyote ile unatakiwa kupata usuluhishi wa watu wawili(baba na mama)
kama walivyoanza wakiwa chumbani…watoto/mtoto hawapaswi kujua kinachoendelea
isipokuwa wawaone wazazi wakipendana na kuona furaha ikitawala ndani ya familia.
Hali
ikizidi kuwa mbaya, basi usuluhisi unaweza kufikishwa katika ngazi nyingine za
usuluhishi kama viongozi wa dini,wazee wa familia na ngazi nyingine zinazofaa.
Katika
jamii zetu tunazoishi, hasa kwa kipindi hiki kumekuwa na tabia iliyozoeleka kwa
wazazi kugombana mara kwa mara na kufikia hatua ya kutengana kwa sababu wanazojijua bila ya kujali kuwa wamezaa watoto.
Madhara ayapatayo mtoto kwa wazazi kugombana na kutengana
Hapa
nitatoa baadhi ya madhara yanayoonekana kirahisi ayapatayo mtoto/watoto kwa wazazi
kugombana na kutengana kwa talaka au njia nyingine;
- Mtoto anaweza kujengeka na tabia ya ugomvi-hii ni elimu ya awali kabisa kutoka kwa wazazi wake
- Suala la wazazi kutengana linaweza kuwafanya watoto kuwa njia panda-waende kwa mama au baba kwa sababu hawana chuki na wazazi wao(wanawapenda wote).Endapo wataenda na kukubaliana na mawazo ya mzazi mmoja, mwingine anakasirika na kusema watoto wa siku hizi wanadharau wazazi wao.
- Mtoto anaweza kuondoka nyumbani na kuamua kuishi maisha yake kwa sababu upendo umetoweka nyumbani.Hili humuweka mtoto kuwa huru kufanya lolote kwa sababu ushirikiano wa kumlea umevunjika.Pia ni kichocheo kikubwa cha ongezeko la watoto wa mitaani/watoto waishio kwenye mazingira magumu
- Mtoto anaweza kupoteza muelekeo kimasomo, hii ni sambamba na kushuka kwa taaluma yake au kuacha shule kabisa
- Mtoto anaweza kupatwa na msongo wa mawazo ulio juu ya uwezo wake, hivyo kupoteza furaha na kuwa mnyonge
Tukilitazama
jambo hili kwa upande wa pili; kuna wakati kutengana kwa wazazi kunaweza kuwa
na faida kwa pande zote (mzazi mmoja na watoto).
Kama
alivyoainisha mtaalamu wa masuala ya talaka, divorce Judith Wallerstein
kuwa ni jambo la busara kutengana kwa talaka endapo watoto watapata
mateso ya kihisia,kupigwa au kunyanyaswa kijinsia na mzazi mmoja, au mzazi
mmoja anapokuwa mlevi kupindukia na kusahau majukumu ya familia.
Jamii na wanandoa kwa ujumla
tujitaidi kudumisha mahusiano ili tuwalee watoto kwa pamoja hivyo kuepusha
ongezeko la watoto wasiokuwa na muelekeo, pia watoto wa mitaani.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni