Mwandishi wa Kitabu-Mtazamo Wako Ni Upi?
Ushauri zaidi: +255 754 572 143
Soma SEHEMU YA 1 HAPA
Picha:http://www.hischerishedones.org |
6.EPUKA KUKAA MAZINGIRA YA
UPWEKE…
Upweke hupelekea huzuni na
kupunguza furaha tuliyo nayo.Mazingira ya kujitenga na kuwa wewe ndiyo wewe kwa
kukumbatia mawazo yaliyo hasi na masononeko huikimbiza furaha na kujiona kuwa
ni mkosaji usiyestahili kuwepo duniani.
7.TAMBUA KUWA PESA PEKEE
HAIWEZI KUKUPA FURAHA MAISHANI
Natumaini unakubaliana na
mimi kuwa si kila mwenye pesa ana furaha wakati wote.Sawa! pesa ni sabuni ya
roho kama walivyosema wahenga, lakini si kiashiria cha kumuweka mtu katika
nafasi ya kuwa na furaha.Mtu aweza kuwa na pesa nyingi lakini akapungukiwa
furaha. Hii ina maanisha kuwa pesa ni kitu kinachofuata baadaye baada ya kitu
kisichohitaji pesa kukupa furaha.Bila shaka umeshuhudia jamii za watu waishio
maisha yenye kipato cha chini lakini wana furaha iliyo kifani! Jifunze kutoka
kwao upekee wa maisha walio nao na kuikubali hali halisi ya maisha na kuongeza
juhudi kusonga mbele.
8.JIANGALIE ULIVYO, WEWE NI
WA THAMANI SANA! HAKUNA MWINGINE KAMA WEWE (tumia
hali uliyonayo kwa manufaa na kujiongezea furaha)…
Kama ilivyoelezwa awali kuwa
binadamu tumeumbwa kwa upekee sana na kila mmoja ana uwezo, akili na kipaji kutofautiana
na mwingine ili tufaidiane.Ikiwa mtu hajajitambua uwezo wake kwa jinsi alivyo,
ni vyema kuchukua hatua madhubuti ya kujikubali kwanza na kujitathimini.Vile
tulivyo yatosha kujitumia kujiongezea furaha na uthamani wetu.Ijulikane kuwa,
hakuna mtu mwingine kama wewe.Jitambue, tumia uwezo ulio nao kuanza pale ulipo
kwa kupenda unachofanya na kujiongezea furaha.
9.REKEBISHA TABIA YAKO
INAYOWAKWAZA WENGINE…
Kuwa na mahusiano mema na jamii ya watu waliokuzunguka ni jambo zuri linalochangia furaha yako.Jitahidi kuondoa tofauti ulizo nazo na marafiki au watu wengine ili kuishi kwa amani, hii itakuweka huru na kukuongezea furaha yako.Hivyo basi, chukua hatua ya kujichunguza na kujirekebisha tabia yako iliyo kinyume na utaratibu wa maisha ya kawaida.
10. TAMBUA KUWA SI WOTE
WENYE KUONYESHA MENO NJE (KUKENUA) WANA FURAHA MAISHANI.
Msemo huu wa Kiswahili-"Moyo unaweza kufurahi lakini macho yanalia" ni sawa kabisa na kinyume chake-"Macho yanacheka (kuonyesha furaha ya uso) lakini moyo unalia".Inamaanisha kuwa mtu aweza kuonyesha furaha ya uso kumbe moyoni ana chuki na majonzi au hasira.Hivyo, usiigize furaha kwa kuonyesha meno pekee ukajiita una furaha ya kweli, jitathimini na utafute au kufanya mambo yatakayokupa furaha ya kweli-furaha ya uso na ile ya moyoni.
Nakutakia kila la heri kurudisha furaha iliyopotea au inayoelekea kupotea kwa kufuata mambo 10 niliyoainisha kwa kina.
Nakutakia kila la heri kurudisha furaha iliyopotea au inayoelekea kupotea kwa kufuata mambo 10 niliyoainisha kwa kina.
Imetolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni