Siku ya mazingira duniani huadhimishwa Juni 5 kila mwaka.
Picha:Mandhari inayotakiwa kwenye mazingira kutoka cerpa.appstate.edu |
Tukienda sawa na ujumbe wa siku hii,uliotolewa na Shirika la mazingira duniani-"United Nations Environment Programme(UNEP)" usemao; "Think.Eat.Save" yaani kwa kiswahili Fikiri.Kula.Tunza-tunatakiwa kutenda kwa kufuata hatua hizo tatu ili kuyafanya mazingira yetu kuwa mazuri kwa uzalishaji mwingine wa chakula.
Ujumbe huu wa Fikiri.Kula.Tunza umekuja kutokana na kuwepo kwa matumizi mabaya ya chakula yanayokinzana na utunzaji wa mazingira.
Shirika la chakula duniani (FAO) limeainisha kuwa tani bilioni 1.3 za chakula hupotea kila mwaka. Hii ni sawa na kiasi kinachozalishwa katika nchi za kusini mwa jangwa la Sahara.
Wakati huo huo taarifa kutoka (FAO) imeripoti kuwa, mtu mmoja kati ya 7 duniani hulala bila kula na watoto zaidi ya 20,000 walio chini ya miaka 5 hupoteza maisha kwa adha ya njaa.
Kampeni kubwa mwaka huu inakuhamasisha kuchukua hatua kuanzia nyumbani ikiunganisha nguvu ya pamoja ya kupunguza upotevu/uharibifu wa chakula,kutunza pesa,kupunguza madhara katika mazingira kwa ajili ya uzalishaji mwingine wa chakula ulio na tija.
Fikiri.Kula.Tunza-ni ujumbe unaokutia moyo kuwa na ufahamu kuhusu madhara ya utumiaji wa aina mbali mbali za vyakula kwenye mazingira.
Hasa ukizingatia matumizi ya kemikali kwenye vyakula, yamechangia uharibifu mkubwa wa mazingira.Hivyo basi, kabla ya KULA chochote FIKIRI kwanza, na usaidie kuTUNZA mazingira.
FIKIRI! KULA! TUNZA!
Jielimishe Kwanza!
kwa kushirikiana na
http://www.unep.org/wed/theme/
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni