Picha imetolewa kutoka:www.internetmoola.com |
Wafanyabiashara wengi, wadogo kwa wakubwa wamekuwa na mazoea ya kujiuliza "kwa nini wateja hawanunui au kwa nini wateja hawatumii huduma yangu?"
Wakifanikiwa kutengeneza faida na kukuza soko la biashara, hujisahau kabisa kutazama mbinu au viashiria vya kuongezeka kwa faida na kukua kwa biashara zao.
Hapa namaanisha, hushindwa kujiuliza kwa nini wateja wao au watumiaji wa huduma zao wanajaa/kumiminika eneo la biashara au kuhitaji huduma kwa wingi.
Swali hili ni la msingi sana kama unataka wateja wako waendelee kujaa na kuhitaji huduma yako kwa wingi.
Hivyo basi, ukifahamu viashiria vya kukua kwa soko lako na kuongezeka kwa faida;
1) utaweza kuwatunza wateja wako kwa muda mrefu bila kuhamia sehemu nyingine
2) utaendelea kuboresha na kuhifadhi viashiria hivyo
3)utafanikiwa kukuza soko zaidi na kupata faida maradufu.
MFANO HALISI :
Kuna mgawaha maarufu sana, walaji wengi hupendelea kwenda kula.Ni sehemu nzuri sana, huduma nzuri sana, pia kuna sehemu ya kuegesha magari kwa ajili ya wateja.
Mmiliki alishangazwa kuona wateja wakiendelea kujaa siku hadi siku, wakati huo huo faida ikiongezeka maradufu.
Unajua nini alichofanya mmliki huyo wa mgahawa?...kwa kutokujua kwa nini wateja wanajaa kwenye mgahawa wake, aliamua kupanua eneo la biashara kwa kuondoa sehemu ya kuegesha magari...Bashiri, nini kilitokea baada ya hapo...
Tuma maoni yako:
Jifunze,Fahamu, Fanya!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni