"Elimu Expo" ni tamasha liliandaliwa na Elimu Solution na Masoko chini ya udhamini wa Vodacom Foundation kwa lengo la kuwashirikisha wadau wote wa elimu ili kuchukua hatua ya kuboresha kiwango cha elimu nchini ambacho ni sawa na jahazi linalotaka kuzama kabisa.
Tamasha hilo lilichukua siku tatu
kuanzia tarehe 30 Agosti hadi 1 Septemba 2013 mgeni rasmi akiwa Naibu Waziri
wa Elimu Mhe.Philipho Augustino Mulugo (MB).
Kulikuwa na mabanda ya kampuni
mbali mbali zenye kutoa mchango kwa elimu na kutoa mustakabali wa elimu nchini
Tanzania.
Jicho la blog yetu Jielimishe Kwanza! lilitua
moja kwa moja kwenye banda la Kampuni ya "Samsung" na "Vodacom" kujionea
mfumo kwa kisasa wa kufundishia ulio sanjari na Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) waliouita "Samsung Smart School."
- Muwezeshaji kutoka "Samsung" akitoa maelekezo ya mfumo wa utendaji wa "Samsung Smart School"
Ilikuwa ni bahati pia kwa kuwa Naibu Waziri wa Elimu Mhe.Philipho Augustino Mulugo (MB) aliweza kujionea mwenyewe jinsi Teknolojia inavyoweza kuboresha mfumo wa ufundishaji nchini.
- Naibu Waziri wa Elimu Mhe.Philipho Mulugo (MB) akifafanuliwa jambo kuhusu mfumo wa utendaji wa"Samsung Smart School"
Jielimishe Kwanza! inaomba kutoa
rai kwa wadau wote wa elimu (yaani mimi na wewe) kutazama mfumo wetu wa
elimu kwa jicho lingine lenye kuendana na mabadiliko na kukua kwa Sayansi na
Teknolojia.
Hatupaswi kuuogopa mfumo huu mpya wa kujifunzia kwa sababu unakwenda kuboresha mfumo wetu wa elimu kama tutaigundua siri yake.
Sasa umefika wakati
wa "kutenda zaidi na kwa ubora kwa jitihada ndogo" na
si "kutumia jitihada kubwa kwa
kazi ndogo isiyo na ubora."
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni