-->
Picha na www.empowernetwork.com |
Kumekuwa na mazoea kwa jamii za watu wengi
hasa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara kuchukulia suala la kutunza rasimali
muda kama mzaha au kitu fulani cha kuchezea na kupuuzia. Hili ni tatizo, lazima
tukubaliane kutokukubalina! ili kubadili mtazamo uliopo.
Nilipoanza kujifunza jinsi ya kutunza muda kupitia watu wanaotunza muda na kujisomea vitabu mbali mbali niligundua siri kubwa katika utunzaji rasilimali muda.Kwa sasa naweza kufanya mambo mengi katika ratiba niliyojiwekea.Nimetenga muda maalum pia kukuandikia ndugu msomaji ili nawe upate kupona na ugonjwa huu ambao unaonekana ni wa kawaida ilihali unateketeza uchumi wa mtu mmoja na taifa kwa ujumla.
Ifahamike kuwa muda ni rasimali kama rasimali
nyingine mfano madini…endapo utatumika vibaya ni dhahili kabisa tutarudi kwenye
ule usemi usemao “majuto ni mjukuu.”
Nikichukulia mfano jijini Dar es salaam nchini
Tanzania, utakutana na watu wenye visingizio kadha wa kadha kuhusiana na
utunzaji wa muda…wengi wamekuwa wakichelewa kuripoti kazini na kusababisha
huduma nyingi kutotolewa kwa wakati, kubwa likiwa foleni barabarani.
Unaweza kuweka ahadi na mtu akiwa yeye ndiye
alipendekeza muda na siku wa kukutana, chakushangaza anakuwa wa kwanza
kuchelewa kufika eneo la ahadi na kuanza kutoa visingizio.
Pia kuna makundi ya watu wengine wajulikanao
kama wapoteza muda…wanajisifu kabisa kwa kusema; ah! tupo hapa tu tunapoteza poteza muda.” Wengine
wanatumia muda vibaya kwa kupiga soga na kusengenya wengine.
Tunaweza kuhama hapo kwa kufuata na kufanya mambo 10 yafuatayo:
1. JIWEKEE
MPANGO WA SIKU WENYE MANUFAA UNAOWEZA KUUTEKELEZA KWA WAKATI HUSIKA
2. TAMBUA
KUWA RATIBA YA KESHO HAIPANGWI KESHO ASUBUHI…INAPANGWA KABLA YA KULALA
3. TUMIA
SIMU YAKO KUKUKUMBUSHA MAJUKUMU YA SIKU NA MUDA HUSIKA
4. UNAPOWEKA
AHADI NA MTU HAKIKISHA UMETATHIMINI MUDA UTAKAOTUMIKA UKIWA NJIANI…UTAEPUKA
KUSINGIZIA FOLENI
5. JIJENGEE
HALI YA UAMINIFU KATIKA KUTIMIZA AHADI KWA WAKATI
6. JIJENGEE
TABIA KUSOMA VITABU VYENYE MANUFAA ILI KUEPUKANA NA KUPIGA SOGA
7. THAMINI
MUDA WA WENGINE…TAMBUA KUWA WANA MAJUKUMU
8. TAMBUA
KUWA UNAPOHARIBU RATIBA YA MTU MMOJA UMESABABISHA WATU WENGINE WENGI KUHARIBU
RATIBA ZAO
9. KUWA
MTU WA MFANO KUJALI MUDA MARA KWA MARA, WENGINE WATAKUIGA
10. USIAMINI
SANA KUHUSU DHARULA…EPUKA KUHAIRISHA HAIRISHA MAMBO YALIYOPANGWA
Nakutakia
mafanikio mema katika kuwa mtu wa kutunza rasilimali muda kwa manufaa yako na wengine.
Imetolewa na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni