Picha na
changeyourfate.org |
Wazazi wengine wamefikia hatua ya
kuwadanganya watoto wao kuwa “…mimi
nilikuwa nashika nafasi ya kwanza darasani hadi namaliza shule…” hii haijalishi
kwao kuwa wameenda shule au la! Kila mzazi anasema alikuwa anashika nafasi
ya kwanza darasani…mh! Sijui nani alikuwa wa mwisho darasani? Naomba tusifikie hapo, kuna njia nyingine ya kuwaeleza watoto wetu kuhusu shule.
Picha na www.alltreatment.com |
...Inafahamika fika kuwa wazazi wengi
huitaji mabadiko au maboresho katika mfumo wa elimu, lakini hivyo hivyo wanaona
umuhimu wa watoto wao kwenda shule...
Leo naomba uchukue hatua muhimu na rahisi kumueleza mtoto
wako kuhusu shule kama ifuatavyo;
1.ELIMU NI HATUA ENDELEVU MAISHANI
Kwenda shule ni hatua mojawapo-lakini ni hatua ndogo
sana.Ukiwa shule utajifunza mbinu mbali mbali…hii isikufanye ukaacha kujifunza
masuala mengine uyapendayo.Ichukulie elimu kama chaguo la kuboresha kipaji
chako(Tukiamini, pia ni uhalisia kuwa kila binadamu ana kipaji chake).
2.SHULE NI HATUA YA AWALI YA KUAJIRIWA.
Shule inakuandaa kujipatia kipato cha halali, lakini si
lazima kukupatia mali.
3.TAMBUA KUWA SHULE NI SEHEMU YA KUFAULU NA KUFELI
Soma kwa bidii.Pata ujasiri wa kusonga mbele pale unapofaulu
pia pata ujasiri wa kuinuka tena pale unapoanguka(Kufeli).
4.UKIANZA SHULE, JITOLEE KUMALIZA
Jifunze kupambana na changamoto mbali mbali bila ya kukata
tamaa.Tambua kuwa shule ni sehemu ya changamoto.
5.SHULE NI SEHEMU MUHIMU YA KUPATA HABARI
Tambua kuwa walimu wako ni watafiti, tumia taarifa zao, uliza
maswali…fanya majaribio ya mara kwa mara ukitumia taarifa hizo kulingana na
kile unachokipenda.Fuatilia kwa kina taarifa hizo kuliko kutegemea kupata
majibu sahihi wakati wote ili ufaulu mtihani.
6. NI VYEMA UKAONEKANA MJINGA KULIKO KUWA MJINGA
Kama huelewi jambo Fulani, ni vyema kuuliza ili kupata
ufafanuzi.Mwalimu akihitaji mtu kujitolea, jitolee.Watu hujifunza zaidi kwa
kushirikishwa kuliko kukaa kimya ili kuonekana mtulivu.Uwe tayari kufanya
makosa-hii ni hatua ya awali ya kujifunza.Fanya makosa sana.Kuwa na heshima
lakini mchangamfu!
7.CHUKULIA FAIDA YA KUWA MDOGO
Hatua ya utoto ina faida zake, muda wa kutosha hasa baada ya
masomo.Tumia muda huo kudadisi masuala mbali mbali.
8.TAFUTA KUPATA MAJIBU SAHII…LAKINI USIISHIE HAPO!
Tafuta jibu analohitaji mwalimu, lakini hakikisha una majibu
si chini ya mawili.Kuwa na uwezo wa kutafuta majibu zaidi kwa maswali na
matatizo mbali mbali ni njia mojawapo ya kuwa na wigo mpana wa kutatua
matatizo.Maisha bila machaguo ni rahisi sana kuwa taabu.
9.JIAMINI…
Kila mtu ana uwezo wa kuelewa na kupambanua.Alama zako
darasani hazibashiri kile utakachoweza kufanya baada ya shule.Fuata ndoto yako
haijalishi watu wanasema nini…
10.UPENDO WANGU KWAKO NI WA MILELE
Waambie watoto wako, haijalishi alama gani wanapata shuleni,
wao ni wa muhimu kwako.Kumbuka kuwa shule ni kama mchezo wa kupata na kupoteza,
lakini utawapenda milele.
Makala hii imeandaliwa na Jielimishe Kwanza! kwa
kushirikiana na Kitabu kiitwacho “Be Rich
and Happy” kilichoandikwa na Robert Kiyosaki- Sura ya 25, Ukurasa wa 259-261.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni