Kumekuwepo
na jitihada kutoka Halmashauri mbali mbali jijini Dar es salaam katika suala zima la usimamiwaji wa sheria ndogo za usafi wa mazingira.
Jitihada
hizo zote zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na ushirikiano hafifu kutoka kwa
wananchi. Hii inaonyesha kuwa uelewa wa wananchi ni mdogo kuhusu umuhimu wa sheria ndogo zinazowekwa kuhusu utunzaji wa mazingira.Pia usimamizi wa sheria hizo ni hafifu.
Tunathibitisha
ukweli wa jambo hili kutokana na hali halisi ilivyo katika eneo lililopo pembezoni mwa barabara ya Ali
Hassani Mwinyi jijini Dar es salaam kama lilivyotembelewa na Jielimishe
Kwanza! kwa mara nyingine.
Picha kama ilivyotolewa kwenye taarifa ya awali: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/mazingira-juhudi-na-changamoto-za.html |
Itambulike kuwa eneo hili ni la mfano kwetu ili iwe changamoto kwa maeneo mengine nchini!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni