-->
M
|
Picha na plancanada.ca |
ara nyingi wasichana wenye umri mdogo
wamekuwa wakiozeshwa kwa kushurutishwa na wazazi, pia ndugu wa karibu kama njia mojawapo ya kujiingizia kipato na mali.Huu umekuwa ni
utaratibu uliozoeleka sana, na wengine kuchukulia kama sehemu ya utamaduni.
Hali hii isiyo ya kawaida inajitokeza sana katika nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara. Tabia hii mbaya isiyojali haki ya mtoto wa kike imesababishia wasichana wengi kukosa fursa za kuendelea kukua kifikra,pia kushindwa kuendelea na masomo.
Msichana asipopata mahitaji yote hayo
muhimu itamfanya awe tegemezi katika maisha yake yote.Hivyo iwapo mtoto wa kike
ataozwa katika umri mdogo kuna uewezekano mkubwa wa kutojua kusoma na kuandika
au atakuwa amepata elimu ya kiwango cha chini, hali hiyo itamfanya awe mtu
masikini na hataweza kujitetea katika maswala ya ngono na nyumbani ukizingatia
kwamba mara yingi msichana anaozwa kwa mtu mwenye umri mkubwa mara mbili yake, ambaye tayari amekuwa ni mzoefu.
Katika hali hii mtoto huyu wa kike
anakuwa na uhusiano tegemezi,uhusiano ambao mara nyingi huwa ni uonevu hasa
ukizingatia ukweli wa hali ya kiuchumi. Kwa ufupi matarajio juu ya mtoto wa
kike yamedumaa na ndiyo maana watoto wa kike wanapata athari kubwa zaidi
ukichulia kuwa msichana huyu mdogo anatakiwa atoke kutafuta,lakini pia aangalie familia
na kumuhudumia mume, wakati mwingine kukosa haki ya kula matunda ya jasho lake
kwa sababu ya ukatili wa mwanaume.
Binti ambaye ndiye mke, asiye na elimu
ya uzazi anapata shida ya kutambua haki ya kumuwezesha yeye kupumzika baada ya
kujifungua.Hili hupelekea kuwa na watoto wengi ambao ni vigumu
kuwahudumia, matokeo yake ni kuongezeka kwa watoto wa mitaani. Jamii inapaswa kutambua na kubadilika,kujua kuwa jinsia zote zina haki sawa,mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuheshimiwa na kupewa haki zao kama ilivyo kwa watoto wa kiume na wanaume.
kuwahudumia, matokeo yake ni kuongezeka kwa watoto wa mitaani. Jamii inapaswa kutambua na kubadilika,kujua kuwa jinsia zote zina haki sawa,mtoto wa kike na wanawake kwa ujumla wanapaswa kuheshimiwa na kupewa haki zao kama ilivyo kwa watoto wa kiume na wanaume.
Wasichana wadogo wanapaswa kulindwa na tatizo la ndoa za
utotoni pia kupewa fursa ya elimu.
Picha na plancanada.ca |
Ndoa za umri mdogo siyo nzuri na hazitakiwi,madhara yake ni
makubwa kuanzia kwenye familia na Taifa kwa ujumla.
Jielimishe Kwanza! Badilika!
Na Linda Kagemulo, 0654289805, lindakagemulo@gmail.com
Na Linda Kagemulo, 0654289805, lindakagemulo@gmail.com
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni