N
|
apenda kushirikiana nawe msomaji wangu kuhusu
uumbaji wa Mungu ukihusisha na maisha yetu ya kila siku. Aliumba viumbe hai na
visivyo hai, pia alimweka mwanadamu kuwa mtawala wa hivyo vyote.
Kupitia utashi aliopewa mwanadamu, aliweza
kubuni mbinu mbali za kuwatunza viumbe wengine…natumaini tunatimiza lengo la kuwatunza viumbe hao wengine wasio na
utashi.Kama tumesahau basi tukumbuke kazi tuliyotumwa!
Tukirudi katika maisha ya kawaida tunayoishi,
mwanadamu amekuwa akigundua vitu vingi ili kutatua changamoto zinazomzunguka.
Kama upo makini na mdadisi utagundua kuwa
vitu vingi afanyavyo mwanadamu kwa ubunifu ni kama amedurufu kazi ya uumbaji wa
Mungu.
Kuna mifano mingi ya kuangalia; chukulia
muonekano wa umbo la chombo cha usafiri wa anga (ndege) kushabihiana na umbo la
ndege arukaye, matoleo mengi ya magari yanayopagawisha watu na vyombo vingine
vya usafiri hushabihiana sana na viumbe hai alivyoviweka Mungu.
Picha na www.hdwallpaperstop.com |
Picha na www.hdwallpapers.in |
Hapa naomba niseme kuwa hati miliki ya
ubunifu wa mwanadamu anamiliki Mungu na si kama wengine wanavyojisifu na kutamba.
Leo naomba tujifunze kupitia mimea hasa
kutafuta na kuziona fursa mbali mbali katika maisha.
Kisayansi, mimea hutegemea sana mwanga wa jua
kujitengenezea chakula na kumea mwisho kufikia hatua ya kutunza viumbe hai
wengine kama binadamu na wanyama.
Fuatilia kwa makini hatua ya awali ya kuanza
kuchipua kwa mmea: mmea ulio katika mazingira mazuri ya kupata mwanga wa jua
humea vizuri na kuzaa matunda.
Pia mimea iliyo katika mazingira magumu
hujitengenezea mazingira kwa hali yeyote ile ili kuliona jua (FURSA). Mimea
mingine hujitahidi kupanda juu ya mimea mingine ili kuliona jua (FURSA). Je,
mimea ina akili sana kushinda sisi? La hasha!
Mimea iliyo songwasongwa na magugu na
kushindwa kujinasua kupata mwanga wa jua
(FURSA) hudumaa na mwisho kufa.
Je, mimea ina akili sana kushinda sisi? La
hasha!
Tuhangaikie suala zima la kuziona fursa kwa
hali yeyote ile ili tusife kifikra na kiiuchumi kwa kujifunza kupitia mimea.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni