-->
Nikianza kwa
kumnukuu mwanamuziki maarufu wa "Reggae" dunia-Hayati Nesta Robert Marley
almaarufu “Bob Marley” aliwahi kusema katika sehemu ya wimbo wa “Redemption
Song” kuwa “Emancipate yourselves from
mental slavery; None but ourselves can free our mind.” Akiweka msisitizo huo kuwa hakuna mtu
mwingine anayeweza kutukomboa/kukukomboa kifikra isipokuwa sisi wenyewe…au wewe
mwenyewe. ANGALIA VIDEO NA MASHAIRI YA WIMBO HUO KUPITIA
Kama
utatafakari kwa kina utagundua kuwa walio juu kimaendeleo na wenye upeo wa kupambanua mambo hupenda kuwakandamiza walio chini hasa wazubavu na hata kudiriki kupita juu ya
vichwa vyao.
Hata siku
moja hawawapi nafasi walio chini kuchomoza kimaisha, hasa kwa kuwapa msaada ili
waweze kufikiri vizuri na kutenda sawia na wenyewe wanavyotenda.
Hali hii hupelekea
kuongezeka kwa wimbi kubwa la wasio nacho na kuimarika kwa kundi la walionacho.
Sina hakika kama lengo la Mungu kumuumba mwanadamu ni kuwa masikini…la hasha! Nini
husababisha haya yote?
Wabudha wana msemo wao maarufu sana ulio na uhalisia kuwa “What we think, we become.” Wakimaanisha-kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa,
tunanyoonekana na jinsi tulivyo kimaisha ni kutokana na mawazo yetu.Mfano,
tukiendelea kunung'unika sana kuwa nchi hii ni masikini sana na hali kuna
rasilimali nyingi hadi wengine wanakuja kugombania…ndivyo ilivyo na
itakavyokuwa!
Kiujasiri
kabisa, ndugu msomaji, nikutie moyo kuwa tukibadili mtazamo wetu wa kufikiri na
kuepukana na utegemezi wa kufikiri tutaondoka hapo tulipo…hivyo kuacha kuimba
wimbo huu wa “Nchi yetu ni masikini sana”
ambao walio nacho wanaupenda sana kuuimba na kuucheza wakati huo huo
wengine-wasio nacho kusikia kelele ndani ya masikio yao na kusononeka mioyo
yao.
Tunatakiwa
kuamini, kufikiri tofauti na kuangalia tulicho nacho kwanza-mfano kipaji au uwezo wa
asili tuliopewa na Mungu kuwa kianzio cha mtaji wetu sambamba na kulinganisha na rasilimali tulizo nazo kusonga mbele.Kuna
uthibitisho kutoka kwa wengine walioiona siri hii ya kutumia kile walicho nacho
kwanza. Jielimishe Kwanza! Jitambue! Fuatilia! Simamia kwa kutenda!
Tusipende kuwa
bendera fuata upepo na kutumika na hao wanaotukandamiza…hata siku moja hawawezi
kutukomboa kifikra.
Huu ni mtazamo
wa Jielimsihe Kwanza! Tunakutakia kila la heri katika kubadili mtazamo kuwa
chanya!
Imetolewa na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni