Katika pita pita za kuchunguza usimamizi wa
sheria ndogo za kulinda na kutunza mazingira zinazowekwa na Halmashauri mbali
mbali kwa ushirikiano wa wananchi nchini Tanzania, Jielimishe Kwanza! ilifanikiwa kujionea hali isiyo ya kawaida pembezoni mwa bara bara ya Ali Hassani Mwinyi jijini Dar es salaam.
Pichani ni bango linalojieleza vizuri kabisa…ikiwa ni amri kutoka katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kudhibiti utupaji ovyo taka katika eneo husika. |
Kuna maswali ya msingi ya kujiuliza…je,
matangazo/vibao vya kutoa onyo vinaendana na utekelezaji? Je, kuna
ufuatiliaji/usimamiaji wa sheria mara tu
baada ya kuweka vibao/matangazo ya onyo?Au ni wakati gani sheria hizo ndogo huwa na meno?...usiku au mchana?...wakati wa ugeni mkubwa au la? Hapo unaweza kulinganisha matokeo ya ukiukwaji au utekelezwaji wa sheria hizo ndogo.
Ifahamike kuwa, kama hakuna ufuatiliaji/utekelezaji wa onyo
zinazotolewa, hali huwa mbaya zaidi ya mwanzo…mwanadamu akipewa onyo halafu
asione utendaji/madhara ya kukiuka onyo, hupuuzia onyo hilo na kuchukulia hali kimazoea.
Ushauri wetu namba 1, tunashauri...mabango/vibao vya onyo vieleze aina ya
adhabu atakayopata mtupaji taka katika eneo husika…Hasa adhabu ya fedha
taslimu.Pia ni vyema kutumia ufuatiliaji shirikishi/jamii kwa kutoa motisha ya nusu
ya fedha taslimu itolewayo kama adhabu kwa watoa taarifa ya uchafuzi wowote wa mazingira.Hii inaweza kuwa chanzo cha mapato kwa mtoa taarifa na Halmashauri husika kwa ujumla wakati huo huo jiji liking'ara.
Ushauri wetu namba 2, tunashauri kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya kutupa taka na kuwe na ufuatiliaji wa mara kwa mara kuhakikisha taka hazirundikani kwa muda mrefu.Kwa kutumia mapato ya ushauri namba 1...yanaweza kuboresha huduma ya ushauri namba 2.
Soma mfano wa kuigwa wa mbinu za
kuhifadhi mazingira kupitia mji wa Moshi uliofanikiwa katika kusimamia
sheria ndogo ya uhifadhi wa mazingira http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/08/mazingira-hii-ndiyo-siri-ya-usafi-wa.html
Jamii kwa ujumla inapaswa kujua uhalifu na uchafuzi wa mazingira wa aina yoyote ile una athari kubwa kwa kila mwanadamu...tushirikiane kwa pamoja kuipendezesha dunia hii inayotutunza.
Imetolewa na,
Jielimishe Kwanza!
Kwa kuthamini umuhimu wa mazingira safi kwa afya bora!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni