T
|
unapozungumzia
suala zima la afya bora ni hali ya kuwa vyema kimwili bila kuwa na ugonjwa au
dalili ya ugonjwa.Watu wengi hujipongeza sana kwa kuamini kuwa afya ni unene…la
hasha!
Afya bora hujengwa/huboreshwa na makundi ya
vyakula yenye virutubisho kama wanga,protini,vitamini, madini, mafuta, maji
safi na salama.
Ukosefu
wa lishe bora na ulaji mbaya umepelekea matizo mbali mbali kwa watoto na watu
wakubwa.
Ukosefu
wa kipato hupelekea kukosa lishe bora na wakati huo huo kuwa na kipato kikubwa
hupelekea kuongezeka kwa uzito wa mwili uliyokithili sambamba na magonjwa
yasiyoambukiza kama kisukari,kansa na matatizo ya moyo.
Je,
ulaji wako ni upi kwa kuzingatia mchoro ufuatao…A au B?
Jichunguze kwa makini, jiweke katika mfumo husika wa ulaji...A au B, Jiulize, hivi nilivyo kiafya
ni sahihi kulingana na kanuni za ulaji bora? Ikiwa si sahihi, Jielimishe Kwanza
kwa kuuliza wataalamu wa lishe,soma vitabu, makala na majarida muhimu kuhusu afya.
Ikiwa hujanielewa, usisite kuniandikia au kunipigia simu...nitakuelewesha.
Nakutakia
kila la heri katika zoezi hili muhimu la kuboresha afya yako na wengine.
Imetayarishwa
na kutolewa na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni