-->
-->
K
|
atika kufuatilia kwa ukaribu tabia na mazoea ya watu mbalimbali jijini
Dar es salaam kwa suala linalohusu afya, Jielimishe Kwanza! imegundua na
kusikitishwa kuona watu wengi huchemua/hupiga
chafya bila kutumia kitambaa safi ili kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi ya
magonjwa yasambaayo kwa hewa kama mafua na kifua kikuu.
Naomba radhi kwa maneno makali nitakayoyatumia…ni kwa lengo zuri tu la kukumbushana na
kuelimishana!
Wapo wanaotumia mikono yao kuzuia
kusambaa kwa mate na makohozi au kushika pua kutoa kamasi na mara tu wakimaliza
hutumia mkono kusalimiana na wengine…kwa kweli hii si nzuri kiafya.
Sambamba na kuchemua na kukohoa,
wapo watu wengine hutema makohozi, mate hovyo bila kuzingatia kuwa kuna
mtu/watu jirani yake.Kiuhalisia, tabia hii si nzuri kiafya na mazingira kwa
ujumla.
Si lazima kwenda shule sana
ndipo ijulikane kuwa kutumia kitambaa safi kufunika pua na mdomo ni muhimu kwa
afya…utajisikiaje kuona mtu mwingine akikurushia mate/makohozi usoni kwa
chafya? Ikiwa hatupendi kufanyiwa hivyo, tusiwafanyie wengine. Hili ni suala la
uelewa tu, halihitaji kuwa na shahada.
Picha na news.discovery.com |
Ikiwa una mazoea tajwa naomba
uchukue hatua ya kubadika na kuwahamasisha wengine kubadilika.
Jali afya ya wengine kama
unavyojijali, Punguza kuenea kwa magonjwa yanayoenezwa kwa hewa.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni