1.Utakuwa
tayari kupokea kila sharti utakalopewa na huyo mlinzi wa SIRI yako.
2.
Wakati wote utaishi kwa mashaka mashaka.Utahisi: labda SIRI ataivujisha nini? Vipi SIRI ikivuja itakuwaje? Nitaweka wapi
uso wangu?
3.Hofu
itatawala, kila umuonapo mlinzi wa SIRI yako.Utahisi: labda anataka kusema kitu fulani kuhusiana na SIRI yangu nini?
4.Utajikuta
ukitumia pesa kinyume na utaratibu ili kuilinda SIRI isivuje.Mlinzi wa SIRI
yako asikohoe kidogo tu kuhusu shida ya pesa, utampatia!…utahisi kuwa usipompatia atavujisha SIRI.
5.Utakuwa
mtumwa tu! hasa ukimwona mlinzi wa SIRI yako akiwa na rafiki zako wa karibu
wakijadili jambo na kucheka ukitazama. (Ilihali wana mambo yao mengine tu) Utahisi:
Ameshawaambia SIRI yangu…
Kuhusu SIRI, msemo huu wa Kiswahili
unatawala-
“Hakuna
SIRI ya watu wawili”.
Pia
hatupaswi kutawaliwa na hisia kupita kiasi!
Kwa wale wasioweza kukaa na SIRI zao-wanaona
zinawawasha, tuungane siku kama ya leo ili nikujuze njia sahihi ya kumweleza
mtu mwingine SIRI yako na usipatwe na hayo 5 niliyoyaainisha.
Imetolewa
na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni