Katika kitabu chetu
kinachofanya vizuri sokoni cha-Mtazamo
Wako Ni Upi? Mtazamo Wako, Maisha Yako Na Mwandishi makini Henry Kazula
ananukuliwa akisema; “Mtazamo ulio nao
kukuhusu ukilinganisha na ule wa wengine unakuwa uhalisia wako kama utaamini”
una mantiki kubwa hasa katika kuamini kuwa mtazamo tulionao unakuwa halisi
katika maisha yetu kama tutajilinganisha na wengine. Mfano: ikiwa kimtazamo
tutaamini kuwa wote waliofanikiwa wamepitia “njia
za panya”; ndivyo itakavyokuwa! Hivyo utajijengea mtazamo hasi kuwa watu
wote waliofanikiwa wana mafanikio yasiyo halali, ilhali kuna njia kem kem za
halali kufikia mafanikio maishani.Mtazamo huo hutufanya watumwa wa mtazamo wa
wengine bila kujijua, yaani kupitia mtazamo huo unaamua hatma ya mtazamo wetu
tusipochukua hatua za makusudi kujifunza kwa makini kupitia hao waliotuzidi.
Hatupaswi kuwa watumwa wa
mtazamo kupitia mtazamo wa wengine tunaowaona wametuzidi kimaisha. Zaidi ya
yote, hatupaswi kuruhusu mtazamo wa wengine uamue hatma ya mtazamo wa maisha
yetu.
Tunapaswa kujijengea mtazamo
wetu ulio thabiti kupitia kujifunza kutoka mtazamo wa wengine kutuhusu kwa
kuzingatia kuundwa kwa falsafa binafsi ya
maisha yetu. Hii inamaanisha kuwa; mtazamo
wetu ulio “jicho la rohoni” kama
ilivyo kwa dhamiri –“sauti ya ndani” huunda falsafa binafsi ya maisha yetu.
Jim Rohn-mmoja wa waandishi na
msemaji mashuhuri wa hadhara duniani anaainisha ukweli na umuhimu wa kuwa na falsafa binafsi ya maisha kwa kusema; Jijengee
falsafa ya maisha yako-“philosopy of life”
ikiwa ni dira inayosimamia, kutawala na
kuongoza maisha yako.Pia hutuepusha na hatari mbali mbali ikiwa sambamba na kuingia
kwenye mkenge wa kutawaliwa na wengine kifikra na kimtazamo.
Swali la msingi kujiuliza
ndugu msomaji; je, tunaimarishaje mtazamo
wetu ili kujijengea falsafa binafsi yenye mafanikio maishani? Ikiwa
unahitaji kutoka hatua moja hadi nyingine ya kimtazamo kuwa chanya kwa
kuzingatia uundwaji wa falsafa binafsi
hauna budi kuzingatia yafuatayo;
1.KUSOMA VITABU
Ni ukweli usiopingika kuwa
kusoma vitabu mbali mbali ili kujitambua kunachangia kujenga mtazamo thabiti
unaopelekea kujijengea falsafa binafsi ya
maisha.Hii ni njia nzuri kuweza kujua mtazamo wa wengine kukuhusu wewe na
kujitathimini kujenga na kuimarisha mtazamo wako.Soma hii kufahamu SIRI iliyopo ndani ya vitabu.
2.NI
VYEMA KUHOJI KWANINI
Soma
hii
kujifunza kuhoji kwanini….
3.JIFUNZE
KWA UZOEFU BINAFSI
Jifunze kupitia makosa.Soma
hii
4.JIFUNZE
KWA KUTAZAMA WENGINE
Njia mojawapo ya kujifunza
ni kuwa mtazamaji mzuri wa yale yanayotokea kwa wengine.Utagundua makosa yao na
mbinu walizotumia kuondoa makosa.Kupitia njia hii utajifunza mbinu mbali mbali
kutoka kwa watu tofauti kuimarisha mtazamo wako.
5.CHUKUA HATUA YA
UJASIRI KUTUMIA MBINU ULIZOJIFUNZA KWA VITENDO
Kujifunza
bila vitendo ni sawa na kutojifunza kabisa.Soma
hii kujua zaidi.
____________________________________________________
Wakati
mwingine nitajikita kwa undani kuelezea kuhusu “Kujijengea Mtazamo na falsafa binafsi ya maisha yako-“philosopy of life”.
Imetayarishwa na,
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni