Picha na www.trinityp3.com |
Wengi hujiuliza, mimi nikiwa
mmoja wao; hivi utendaji kazi wangu
unaendana na matakwa ya mwajiri au malengo ya kazi niliyojiwekea? Wengi wao
hushindwa kupata majibu sahihi kupitia uhakiki au tathmini binafsi “self- assessment” kutokana na
kukosekana kwa mbinu stahiki. Hii imepelekea wengi kuwa tegemezi kwa kupata
tathmini zisizokidhi kiu zao kutoka kwa wengine kuhusu utendaji kazi wao; ingawaje
ni jambo jema pia kupata tathmini ya wengine kukuhusu na kuhusu utendaji kazi
wako.
Kutegemea tathmini ya
wengine pekee kuhusu utendaji kazi wetu inaweza isiwe njia sahihi zaidi kuliko ile binafsi-“self assessment” kutokana na kuwepo
kwa ubinafsi/ unafsi na roho za korosho
au roho za kwanini yeye? baina ya
mfanyakazi mmoja na mwingine, kadhalika kati ya mfanyabiashara mmoja na
mwingine.Hakuna anayependa mafanikio ya mwingine katika utendaji kazi na
biashara.
Katika karne hii ya
utandawazi iliyo na mabadiliko kila kukicha, bila kusahau ubunifu wenye ushindani mkubwa -ujulikanao kama "creative destruction" kama alivyowahi kuainisha Joseph Schumpeter (1883–1950), ni muhimu kutambua kuwa upo
umuhimu mkubwa wa kujitathmini mwenyewe
kiutendaji ili kuboresha mapungufu uliyo nayo kwa haraka zaidi ukiendana na
uhitaji wa soko la ajira au biashara.Ubunifu wenye tija unahitajika sana katika wakati huu tulio nao.
Kwa bahati nzuri sana;
kumekuwepo na tafiti mbali mbali zinazohamasisha kujifanyia tathmini binafsi ya
kiutendaji kabla ya kuomba ridhaa ya wengine kututathimini. Michelle Roccia,
mtendaji msaidizi wa kitengo cha “Employee
Engagement” katika kampuni ya WinterWyman anasema; “The self-assessment is an essential part of performance evaluation
because it's an opportunity for you to assess your own achievements. You own
the performance appraisal. You should look across the past year and tell your
manager what you've done and areas you'd like to focus on," Anasisitiza
kuwa tathmini binafsi ya kiutendaji ni fursa kwako kujua maendeleo na mafanikio
katika utendaji kazi wako.Pia ni kipimo cha utendaji wa kazi au biashara
yako.Kwa kuzingatia mwaka uliopita unaweza kujionea ni maeneo yapi unayopaswa
kuweka maboresho na msisitizo zaidi ili kuongeza uzalishaji.
Ford Myers, mwandishi wa
kitabu "Get
The Job You Want, Even When No One's Hiring anaongezea tena kwa kukazia
fikra kuhusu “self-assessment” akisema
kuwa; "It's an opportunity for you
to reflect on how you're doing in your career, not just your job".Use it
to think about where you are going long-term and where you are in your career. Akimaanisha
kuwa; tathmini binafsi ni fursa kwako kuvuta taswira ya jinsi unavyofanya
katika ujuzi na utendaji wako na si kazi pekee. Itumike kutafakari kwa kina
kuhusu mwenendo wako kiutendaji na wapi ulipo kiutendaji.
Pia tathmini binafsi hupelekea kujiongezea sifa katika soko la ajira-bringing value to the market place; kama
alivyosema Jim Rohn. Mtu binafsi kwa
kufanya tathmini binafsi anaweza kujifunza mbinu mbali mbali za kujiongezea
utendaji kazi zinazohitajika katika soko la biashara au ajira kutokana na mapungufu
au uhitaji alio nao.
Ukizingatia faida tajwa za
kujifanyia tathmini binafsi ya kiutendaji, ni vyema kuanza sasa kuangalia wapi
ulipo katika utendaji kazi wako; ikiwa unafanya kazi bora upate ujira pekee au
unafanya kazi ili kujiongezea fursa za kupata pesa zaidi; utaamua wewe.
Nimeandika makala hii kwa makusudi kabisa
ikiwa ni sawa na “kurusha jiwe kwenye giza
nene”; yeyote atakayepiga kelele huko, limempata kwa nafasi yake
kiutendaji.Utaangalia ni eneo gani upo katika utendaji kazi, hivyo anza sasa
kujitathmini mwenyewe, usisubiri kuambiwa na wengine kwa kupakwa mafuta kwa mgongo wa chupa. Najua kuna swali mahsusi
unataka kuuliza tena; nawezaje kujitathmini
mwenyewe? How can I make self -assessment?
Ungana nami wakati mwingine kama huu
utajibiwa bila hiyana ikiwa tu utaniandikia kuhusu kuguswa na makala hii.
Whatsapp +255(0) 754 572 143
Imetayarishwa
na
Mwandishi
wa Kitabu-“Mtazamo Wako Ni Upi?”
Imetolewa
na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni