“ …Kufanya biashara
yenye mafanikio si kutegemea kuona mafuriko ya pesa kwa mkupuo; ila ni
kukusanya faida/pesa kidogo kidogo kutoka vyanzo vidogo vidogo vya mapato”
-Bw.Baraka
Mponda-
______________________
Tunapozungumzia kilimo cha
kijasiriamali ni kilimo kinachofanyika na kufanikiwa katika mazingira yenye
changamoto ambazo hubadilishwa kuwa fursa. Mkulima mvumilivu na makini huona na kuitumia fursa ambayo wengine hawajaiona au wameiona na kupuuzia.
Jicho la blog hii kimtazamo
liliweza kumuona mkulima makini na mjasiriamali mwenye mafanikio Bw. Baraka Mponda (44) wa kitongoji cha
Patandi, Tengeru-Mita chache kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Nelson Mandela -Arusha anayejihusisha na kilimo
cha kijasiriamali cha mboga mboga na viungo. Alianza kujihusisha na kilimo mnamo mwaka 1992 katika
eneo la nyumba yake ambalo tumemkuta.
Bw. Baraka Mponda (44) akielezea jambo kwa mwandishi-Henry Kazula kushoto kwake. |
____________ _________
Yafuatayo ni mahojiano yetu na Bwana Mponda ikiwa ni hamasa kwa vijana na wakulima wengine wenye kianzio lakini wanashindwa kuchukua hatua nyingine ya kiujasiri kuondoa changamoto na kuzibadilisha kuwa fursa.
Mahojiano yalianza hivi:
·
Je,
ni shughuli hii hii ya kilimo cha kijasiriamali cha mboga mboga na viungo,
ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na kuku wa kienyeji imekufikisha katika mafanikio
tunayoyaona leo? Ukizingatia kuwa unauza mboga kwa shilingi 100 kwa fungu moja!
“ …Kufanya biashara
yenye mafanikio si kutegemea kuona mafuriko ya pesa kwa mkupuo; ila ni
kukusanya faida/pesa kidogo kidogo kutoka vyanzo vidogo vidogo vya mapato” …
alisema Bw.Baraka Mponda kwa kujiamini.
alisema Bw.Baraka Mponda kwa kujiamini.
·
Ni lini
umeanza kujishughulisha na kilimo cha kijasiriamali na kiutaalamu kwa mfumo wa
umwagiliaji matone-“drip irrigation”
kupitia njia ya “pump” na kisima
ulichochimba.Vipi ulitumia gharama kiasi gani kwa huu mfumo wa “drip
irrigation”?
…Mfumo
huu wa kilimo cha kijasiriamali cha-“Drip irrigation” nimeanza mwanzoni mwa
mwaka 2015 kwa gharama ya shilingi milioni 5, ingawaje nilianza kujishughulisha na kilimo cha mboga mboga na viungo mnamo mwaka 1992.
Mipira ya kutandaza kwenye
matuta iliyounganishwa katika mfumo wa maji ya kisima cha kuchimba mwenyewe na
“pump” nimenunua kutoka kampuni ya “Bulton Tanzania Limited” kwa
teknolojia kutoka Israel...Alisema Bw.Mponda.
Mfumo wa umwagiliaji katika shamba la Bw. Baraka Mponda (44) nyumbani kwake. |
·
Unaweza
kuelezea jinsi ulivyoweza kuchimba na kuhifadhi maji kwenye "reservoir"; umetumia
gharama kiasi gani?
…Chanzo
cha maji kwa matumizi ya nyumbani na kilimo ni kupitia kisima cha kuchimba na
kuhifadhi maji kutumia “pump” katika “tank” na “reservoir” yenye ujazo wa
36,000ml. Zoezi zima la kupata maji limenigharimu shilingi milioni 7…alisema kwa
ujasiri Bw.Mponda.
Nyumba ya Bw. Baraka Mponda (44) inavyoonekana katika mwinuko ilipo "reservoir" kwa ajili ya kilimo. |
·
Nini
mafanikio yako tangu uanze kujihusisha na kilimo cha kitaalam na kijasiriamali?
…Mimi
ni baba wa watoto 3, nina uwezo wa kuwahudumia watoto wangu kwa kila kitu ikiwa pamoja na kielimu hadi ngazi
ya chuo kikuu. Mtoto wangu wa kwanza anaenda chuo kikuu mwaka huu, wa pili yupo
shule ya sekondari nzuri na inafanya vizuri kitaaluma. Nina nyumba yangu na Magari mawili; moja la kutembelea mke
wangu na lingine la shughuli za shamba.Pia nimeajiri vijana 3 wanaonisaidia
shughuli za shamba na ufugaji…alijibu kwa tabasamu Bw.Mponda.
·
Je
unajishughulisha na nini kingine zaidi ya kilimo?
Mimi ni msambazaji wa mboga
mboga kwa “tender” katika mahoteli jijini Arusha (shughuli hii inayohitaji kuwa na mtaji wa
shilingi milioni 10).
·
Nini malengo yako ya siku za usoni?
…Malengo
yangu ya baadaye ni kulima kisasa zaidi kwa kutumia “greenhouse” hasa kwa zao
la Hoho nyekundu na Njano…Alisema Bw.Mponda.
·
Kipato
chako cha mwezi ni wastani wa sh.ngapi?
…haina
shida! Kipato changu kwa mwezi hakipungui milioni 2 ikiwa nilianza na mtaji wa
shilingi 10,000 kununua mbegu.
·
Umepitia
changamoto zipi hadi leo tunaona mafanikio yako?Ulifanyaje kupambana nazo?
…Bila
kuficha, hakuna kazi isiyo na changamoto; Kutokuwezeshwa kimtaji; mafanikio
niliyonayo yangeweza kuwa makubwa zaidi na kutoa fursa ya ajira kwa wengine.Kutokata
tamaa/uvumilivu na kuthamini kidogo unachopata ni msingi mkubwa katika kukua
kibiashara.Maisha ni kupambana hata katika mazingira magumu.
· Tumalizie
kwa kutoa ushauri wako kwa vijana na
wakulima wengine:
…Nawashauri
vijana na wakulima wenzangu kuwa na Uvumilivu na kupambana…alijibu kwa kifupi.
·
Nini rai yako kwa wadau wa kilimo na serikali?
…Nasisitiza
utolewaji wa semina na warsha kwa vijana zenye kuwawezesha na kutoa fursa za
kujiajiri katika kilimo. Pia, Serikali inatakiwa iwafungulie vijana milango ya
kujiajiri kwa kumaanisha na isiwe kuongea tu bila utekelezaji…alimalizia
Bw.Mponda.
Picha zote na Paul Lucas- mwanafuzi shahada ya uzamili, Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia-Nelson Mandela.
Imetayarishwa
na
Mwandishi
wa Kitabu-“Mtazamo Wako Ni Upi?”
Imetolewa
na
Jielimishe
Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni