inspire
Lebo
business consultancy
Business consulting-2
Swahili translator
E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?
TANGAZO TUWEZESHANE
DUNIA IKUONE
Jumamosi, 17 Desemba 2016
Jumanne, 13 Desemba 2016
MTAZAMO: SHAIRI: "HATUFUNDISHWI SHULENI"
_______________________________
MTAZAMO:SHAIRI
Na Justine Kakoko
Activities: Social & Political activist I Social entrepreneur
I Administrator I
Poet & Song writer based on
Pan-africanism Ideology
Poet & Song writer based on
Pan-africanism Ideology
E-mail: justinekakoko@gmail.com.
______________________________________
SHAIRI: "Hatufundishwi
Shuleni"
Hutufundishwi Kujiamini/
Hatufundishwi Kujithamini/
Hatufundishwi Kujijua,
Kujitambua Sisi Ni
Wakinanani/
Hatufundishwi Tukagundua
Wapi Tulikuwa Kabla Ya
Ukoloni/ Zaidi Ya
Kuchukiana
Hatufundishwi Kupendana
Darasani/ Hata Sishangai
Nikisikia, Mwafrika Kuingia
Vitani Kisa Dini/
Hatufundishwi Faida ya
Kuungana/ Hatufundishwi
Umuhimu Wa Kushirikiana/
Kuweka Nguvu Pamoja
Biashara Zilete Maana/
Tunafundishwa Ukilema
Watu Wazima Kutegemeana/
"..Aliyeanguka Sio
Wenu.."
Hatufundishwi Kuinuana/
Tunafundishwa Historia
Isiyoandikwa Na Sisi/
Historia Iliyobadilishwa
Historia Isiyonauhalisi/
Tunafundishwa Matatizo
Pasipo Njia Za Kuyatatua/
Inachosha, Yanazidi
Ongezeka
Hakuna Linalopungua/
Hatufundishwi Tukajua Kuwa,
Waafrika Tuna maadui/
Kila Nyakati Twawindwa
Si Usiku Mchana Hata
Asubui/
Mzungu Njama Nyingi
Katu Mapigo Hayapungui/
Tumechomwa Sumu Tumeachwa
Tunatizama Alama Ya Ndui/
Tunafundishwa Kuigiza
Nyendo
Za Mzungu/ Tusichojua
Hayomaigizo
Yanaongeza Ukungu/
Hutufundishwi Mifumo Ya
Dunia/
Jinsi Gani Inafanya Kazi
Ili
Tusije Angamia/ Waongozoji
Kitu Gani Haswa
Walichokipania/
Agenda Zao Wapi
Zilipolalia/
Hatufundishwi Uozo Wa
"Umoja
Wa Mataifa" Nyuma Ya
Pazia/
Hatufundishwi Kwanini
Mashujaa
Wa Afrika Tunaendelea
Kuwafukia/
Tunafundishwa Nadharia Bila
Vitendo/
Tunafundishwa Subira, Eti
Polepole
Ndio Mwendo/ Tunafundishwa
Wagunduzi
Wa Afrika Tuliyoikaa Tokea
Mwanzo/
Mambo Ya Vasco Dagama,
Historia Ya Kitoto
Tufanye Ukatazo/
Hatufundishwi Jinsi Ya
Kujilinda/
Hatufundishwi Jinsi Ya Kuyapinga
Mazito Yanayotushinda/
Hatufundishwi Kukwepa
Propaganda
Kuondoka Kwenye Runinga/
Ili Twende Kusoma Tuondoe
Ujinga/
Hatufundishwi Tukajijua
Kiundani/
Ili Tuwe Imara Kimwili Na
Akili
Yatupasa Tule Chakula Gani/
Hatufundishwi Elimu Ya
Jinsia
Wengi Tunajifunzia
Uwanjani/
Hatufundishwi Mahusiano,
Usione Ajabu Ni Malumbano
Nyumbani/
Hatufundishwi Kwanini
Hakuna
Ajira Nchini/ Tunafundishwa
Ajira
Zipo Tunasoma Kwa
Matumaini/
Hatufundishwi Kujiajiri,
Tumalize
Tuishi Kimasikini/
Hatufundishwi
Kujenga Bila Hofu Ya
Kuanguka Chini/
70% Ya Vijana Wapo Vijiweni
Baada Ya Kuitimu Vyuoni/
Inabidi Iwe Hivyo Maana
Hatufundishi Kipi Kipo
Mtaani/
Hatufundishwi Kwanini Sisi
Ni Masikini/ Masikini Wa
Hali Ya
Chini Maisha Yetu Duni/
Kipi Chashusha Kabisa Hali
Yetu Ya Uchumi/ Mbona
Tunawanyama Tele
Mbugani..?/
Mafuta Na Madini
Yanachimbwa Ardhini...?/
Lakini Hatufundishwi,
Kuuliza Kwanini..?/
Hatufundishwi Kuijenga
Afrika/
Hatufundishwi Afrika
"Mpya"
Nini Inataka /
Hatufundishwi
Kuichukia Misingi
Iliyotuzika/
Misingi Waliyoijenga
Ili Unyonyaji Usijekatika/
Kiukweli Tunafundishwa
Kulala,
Katu Hatufundishwi Kuamka/
Hatufundishwi Kuijua Siasa/
Siasa Inaendeshwa Vipi
Ndani
Ya Ulimwengu Wa Sasa/
Tunachofundishwa Ni Akili
Kuzipumbaza/ Hatufundishwi
Kwa Macho Matatu Dunia
Kuiangaza/
Kuangaza Marekani Na China
Wanavyotuburuza/
Tunahitaji Elimu Yenye
Kuiakisi Afrika/
Itakayotuhusu Sisi Na
Mazingira
Yanayotuzunguka/
Itakayorekebisha Makosa
Ya Wapi Tulipoanguka/
Itakayotuonyesha Njia
Na Vipi Tutainuka/
Itakayoturudisha Kwenye
Asili Mpaka
Tutapojikumbuka/
Elimu Hii Ya Sasa, Elimu
Hii Nimeichoka/
Tunahitaji Tufundishwe
Historia Yetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Tamaduni Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Thamani Na Ushujaa
Wetu/ Tunahitaji
Tufundishwe Wapi Walipoishia
Babu Zetu/ Ili Juhudi Zao
Ziendelezwe Visibezwe
Vizazi Vyetu/ Tunahitaji
Tufundishwe Juu Ya Imani
Na Dini Zetu/
Tunahitaji Tufundishwe
Kutofautisha
Kati Ya Taarifa na maarifa/
Ili Tusioshwe Ubongo, Uongo
Uongo
Usilete Nyufa/
Tunahitaji Tufundishwe
Chanzo
Cha Magonjwa Kama Ebola Ona
waafrika Wanavyokufa/
Tunahitaji Tufundishwe
Kujiongoza
Tuondoke Utumwani/
Tuhitaji Tufundishwe Ili
Tusirudishwe
Mashambani/
Tunahitaji Tufundishwe,
Vipi Izalishwe
Isisafirishwe Katani/
Tunahitaji Tufundishwe
Kupendana
Waafrika/ Chuki Yatutafuna,
Umoja
Hatuna Twaingilika/
Tunahitaji Tufundishwe
Manufaa
Ya Elimu Tuipatayo/
Elimu Tuipatayo Ituondoshe
Kwenye Hali Tulionayo/
Elimu Tuipatayo, Ikamilishe
Safari
Tuijengayo/
Elimu Tuipatayo Ilishe
Wengi
Isiache Wengine Wapige
Mwayo/
Tunahitaji Tufundishwe Wizi
wa Warumi Na Wagiriki/
Kubeba Kila Kilichochetu
Kusema
Chao Wakadiriki/
Dini, Sanaa, Sayansi,
Uandishi,
Vyote Tulianzisha Sisi
Hawatuandiki/
Tunafundishwa Uongo,
Lakini, Ukweli
Haubadiliki/
Tunahitaji Tufundishwe Haki
Zetu Za Msingi/
Ili Uonevu Uondoshwe Maana
Manyanyaso Ya Polisi Ni
Mengi/
Malcolm X Alisema,
"Hakuna Mtawala
Anayemfundisha
Mtumwa Kuwa Huru"
Basi Tufundishane Kuikata
Minyororo
Ikiwa Kweli Tunauhitaji
Uhuru/
-GSP
KUSIKILIZA SHAIRI "Hatufundishwi Shuleni" na
MASHAIRI MENGINE, JIPATIE CD YAKO-VOL 1-
TZS 6,000
+255 754 572 143
Jumamosi, 26 Novemba 2016
Tangazo: GO-GREEN-EXPO
Please take our apology for extending this important event of our time to 25th-26th March 2017.This is in response to make it more appealing and involve more stakeholders as agreed with some sponsors.
Doors for Exhibition registration with bonus and Sponsorship or Involvement are open till 30th December 2016.
You are welcome to showcase your Green/Sustainable business!
Karibu sana.Dar es salaam, Tanzania
Info: +255 754 572 143
More updates, please follow:
#gogreentanzania #JielimisheKwanza #TGBN #SDGsActionTanzania
Info: +255 754 572 143
More updates, please follow:
#gogreentanzania #JielimisheKwanza #TGBN #SDGsActionTanzania
Jumapili, 30 Oktoba 2016
Ijumaa, 14 Oktoba 2016
Jumanne, 30 Agosti 2016
Jumanne, 16 Agosti 2016
Ijumaa, 12 Agosti 2016
SIKU YA VIJANA DUNIANI 2016
“Activista Tanzania” Yawakutanisha Vijana Jjijini Dar es salaam
Kujadili Jinsi Ya Kuondokana Na
Umasikini Na Jinsi Ya Kuwa Na “Uzalishaji
Endelevu Na Matumizi Yenye Tija, hii
ikiwa ni kauli mbiu ya mwaka 2016 kwa siku ya vijana Duniani.
Ndugu Hatibu Kilenga, Mwenyekiti wa Activista Tanzania akifafanua jambo kuhusu ushiriki wa vijana
katika maendeleo.(Picha na Activista
Tanzania)
Vijana wakifuatilia mada. (Picha: Activista Tanzania)
Kipekee, kwa kuzingatia
mchango kwa vijana na nguvu yao katika jamii, Henry Kazula- Mkurugenzi wa kampuni ya “Jielimishe Kwanza” alipata fursa ya kuhudhulia tukio hilo na kuwa
miongoni mwa wawezeshaji kwa kutoa mada kuhusu lengo namba 12 kati ya 17 la
Maendeleo Endelevu: “Matumizi Endelevu na Uzalishaji wenye tija” (Sustainable Consumption and Production).
Henry Kazula- Mkurugenzi wa kampuni ya “Jielimishe Kwanza” akitoa mada
kuhusu “Matumizi
Endelevu na Uzalishaji wenye tija”-lengo namba 12/17 Maendeleo endelevu ya
dunia 2030.(Picha: Activista Tanzania)
Washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha na Activista Tanzania).
Imetolewa na Jielimishe Kwanza Blog
Washiriki wote wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha na Activista Tanzania).
Imetolewa na Jielimishe Kwanza Blog
Jumamosi, 6 Agosti 2016
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)