inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 19 Mei 2016

BIASHARA: MAMBO 5 NYETI YANAYORUDISHA NYUMA UKUAJI WA BIASHARA YAKO


Photo: John Mbanda
Kama ilivyo ada, wafanyabiashara wengi; wakubwa kwa wadogo, nchini Tanzania na kungineko duniani hupenda husimamia kukuza soko(ongezeko la wateja) na kujiongezea faida. Si jambo la kubeza hata kidogo kuwa ongezeko la faida litokanalo na ongezeko la wateja ni msingi wa kukuza biashara yako.

Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya biashara mpya 100 zilizoanzishwa ni 5 pekee hudumu kwa miaka 5 na nyingine hufa katika kipindi cha miezi 6 ya utendaji, nyingine kati ya miaka 2 na nyingine miaka 3.

Wakati huu, yamezekana nimekuandikia makala hii wewe uliye na Kampuni/Biashara yenye umri zaidi ya miaka 3 na bado ipo vile vile ….yaani wewe ni kutembeza nguo miaka nenda rudi (Mfano wa mfanyabiashara mdogo).Vipi siku nguvu zikiisha za kutembea kwa miguu?, ikiwa ni hivyo kuna tatizo na unapaswa kujiuliza kwanini biashara yako haikui.

Mara nyingi napenda kusisitiza kupitia msemo maarufu wa Kiuchumi kutoka kwa Jim Rohn kuwa “People get paid for bringing value to the marketplace”…yaani kwa tafsiri ya Lugha ya Kiswahili; Watu hulipwa kutokana na uthamani wauletao kwenye soko.Soko linalozungumzwa hapa ni “watu”; ni kukidhi maumivu ya wateja/ uhitaji wa wateja.

Katika harakati za kukuza wigo wa biashara, iwe kubwa au ndogo, kuna mambo ya msingi sana ya kuzingatia. Haitoshi kuendelea kuzalisha/ kuuza bidhaa au kutoa huduma bila kuzingatia uhitaji wa wateja kwa wakati husika, hivyo kila wakati ni vyema kujua kuwa inampasa mfanyabiashara kujifunza kufanya/kuendesha biashara yake katika mfumo usio wa kawaida wa kimazoea…ni lazima kufanya biashara nje ya mfumo ili kukidhi uhitaji wa soko kwa wakati husika.Ubunifu unahitajika sana! hasa katika mfumo huu wa soko huria wenye ukuaji wa kasi wa teknolojia.

Kupitia ufafanuzi huo, yafuatayo ni mambo (5) nyeti ambayo kwa hakika yanarudisha na pia yamerudisha nyuma ukuaji wa biashara nyingi.
1.KUENDESHA BIASHARA KIMAZOEA- Kuamini zaidi katika njia fulani pekee katika kuendesha biashara na kusahau kuwa mahitaji ya wateja yanaweza kubadilika kutokana uhalisia wa maisha kwa wakati husika.

2.KUKOSA UBUNIFU (Kuiga na si kuboresha mapungufu ya wengine)...hivi sasa nchini Tanzania, kila mtu anafikiria kuwa Wakala wa Makampuni makubwa mfano: Simu, Bima na Benki. Simaanishi kuwa ni vibaya, lakini ni vyema kujiongezea ubunifu binafsi.

3.KUDHARAU WATEJA WAPYA (Kuridhika na wateja waliopo kwa kuwa faida inaonekana kwa waliopo).Huku ni Kujisahau au nasema ni kulala fofofo! Ili kuzinduka usingizini, ulizia makampuni haya makubwa  yaliyowahi kuwepo duniani- “Kodak” na “Sony”, yapo wapo? na yanafanya nini kwa sasa? ukilinganisha na uhitaji wa soko na kukua kwa teknolojia.

4. KURIDHIKA NA AINA KADHAA ZA BIDHAA/HUDUMA( kuamini kuwa bidhaa/huduma fulani ndiyo iliyolishika soko, hivyo hatubanduki hapo.Ni vyema kukidhi matakwa kwa wateja kwa wingi kulingana na uhitaji wao.

5.KUDHARAU KUJIHAKIKI, HAKUNA MALENGO YA MUDA MREFU-“Ignoring reinvention”.Tambua kuwa kila baada ya mwaka unaitathmini na kuhakiki biashara yako, kinyume na hapo mambo yanabadilika kwa kasi na unaiweka biashara hatarini.Pia weka malengo ya muda mrefu ya biashara yako yakisaidiwa na malengo ya muda mfupi.

Epuka mambo hayo 5 tajwa ili kukuza biashara yako.

Ushauri zaidi wa Kibiashara: +255 754 572 143
Imetolewa na Jielimishe Kwanza

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni