Author: Mtazamo Wako Ni Upi?
Founder & Executive Director:
Jielimishe Kwanza Co.Ltd,
Blogger: Jielimishe Kwanza Blog
+255 754 572 143
Kampeni ”Save Life. Save Water ecology” –“Okoa
Maisha.Okoa Ikolojia- Maji” ni ya kwanza na ya kipekee kuzinduliwa nchini Tanzania
chini ya udhamini wa kampuni “Jielimishe Kwanza” na “Jielimishe Kwanza Blog”
katika miradi yao endelevu: “Environmental Activists in Tanzania”, “Enviro-Forum” na
“Social & Environmental Entrepreneurship in Tanzania (SEE-Tanzania).
Mr.Henry Kazula, akifafanua kuhusu "Save Life.Save Water ecology"campaign-Tanzania. Picha:Blogs za Mikoa). |
Pia, kampeni hi iliweza kushirikisha kwa ukaribu
Dawati la Vijana-UNESCO “UNESCO-Youth Desk-Tanzania” na mashirikishika mengine yasiyo ya
Kiserikali yajihusishayo na Utunzaji na Usimamizi wa Mazingira kama Comprehensive
Environmental Management Organization (CEMO), “Young Lawyers Foundation” na “Jane Goodall’s Roots&Shoots”
”Save Life. Save Water ecology” -“Okoa Maisha.Okoa Ikolojia Maji” imekuja mahsusi
kutokana na kuwepo kwa athari za mabadiliko ya tabianchi (mfano: mafuriko) pia
uvamizi wa maeneo yaliyo kando kando ya vyanzo vya maji kwa shughuli za
kibinadamu ambazo huathiri/huchafua ikolojia-Maji na kuhatarisha maisha ya
viumbe walio majini pia kuyafanya maji yasiwe salama kwa matumizi ya
Kibinadamu.
Kampeni hii endelevu nchini Tanzania imelenga kutoa hamasa kwa jamii kupitia warsha za vyuo vikuu kama “Sauti ya Vijana”, Radio na Televisheni katika kuleta mwamko chanya wa kuhifadhi vyanzo
vya maji na kuutaadharisha umma kuhusu madhara na athari zitokanazo na
mabadiliko ya tabianchi kwa kuishi maeneo hatarishi-hasa mabondeni, katika fukwe
za Bahari, Maziwa na Mito.Kauli mbiu yake ikiwa; “Usiishi mabondeni,katika Fukwe za Bahari,Maziwa na Mito”-Stay out of Valleys,Ocean,Lake
and River shorelines”. Pia, imelenga kushirikiana na jamii katika kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji kwa kupanda miti, kusafisha fukwe za bahari,maziwa na mito.
Hivyo, kupitia Sheria ya
mazingira(2004) inayosimamiwa na Baraza la Taifa la hifadhi
na usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Sheria ya Ardhi Sura 113, kampeni hii imedhamilia kwa dhati kutoa hamasa,
ufahamu, ufafanuzi na taadhari kwa umma kujiepusha kuishi katika “maeneo ya mazingira nyeti” kama
ilivyoainishwa katika Sheria ya Mazingira(2004),sura 191(kif.51) na maeneo
hatarishi katika Sheria ya Ardhi sura 113(6 na 7).Pia kutoa ufafanuzi juu ya
umbali halisi wa kufanya shughuli za kibinadamu kutoka kwenye kingo za bahari,
maziwa na mito kwa kuzingatia EMA,2004 51(1)na (2) ili kuhifadhi vyanzo vya maji kwa maslahi ya kuokoa maisha ya binadamu kutokana mafuriko, kuokoa rasilimali fedha, na kujali maslahi ya utunzaji
Mazingira kwa maendeleo endelevu (Sustainable development).
Shughuli nzima ya
uzinduzi iliyofanyika jijini Dar es salaam tarehe 29-30 Aprili 2016
iliwajumuisha washiriki ambao ni Wanaharakati wa Mazingira na Maafisa Mazingira
kutoka Miji mikubwa- Dar es salaam,Mbeya,Arusha, Mwanza na Tanga; ambayo
Kampeni hii imelenga kuendelea na uhamasishaji; lengo kubwa likiwa ni
kufikisha ujumbe huu mahsusi kwa watanzania wote kwa maslahi ya Kijamii,Kimazingira
na Kiuchumi hatimaye Taifa letu liweze kuyafikia malengo endelevu kwa kuchangia
juhudi za Umoja wa Mataifa za Malengo 17 ya Maendeleo endelevu(17 SDGs ,2030).
Washiriki walijumuika
kujifunza na kubadilishana mawazo juu ya Sheria ya Mazingira 2004-utekelezaji
na changamoto zake.Pia kutoa mapendekezo yatakayowasilishwa katika Baraza la
Taifa la hifadhi na usimamizi wa Mazingira(NEMC).
Kampeni hii iliweza kutoa
na kuboresha ufahamu na ushirikiri wa jamii katika kutekeleza malengo ya
Maendeleo endelevu yaliyo sanjari na uhifadhi wa vyanzo maji na kuokoa maisha
ya watu na viumbe waishio majini.Mmbadala wa ujarisimali jamii na ule wa
Mazingira (Social & Environmental Entrepreneurship) kama “Ecotourism”
ulipewa kipaumbele katika kupambana na uhifadhi wa vyanzo vya maji wakati huo
huo jamii husika ikiboresha uchumi na maisha.
Siku ya pili ya shughuli
ya uzinduzi wa kampeni hii; washiriki, kwa kuonyesha nia ya dhati ya kujifunza
na kujionea uhalisia wa shughuli za binadamu katika uchafuzi wa mito na bahari,
waliweza kutembelea Mto Mbezi. Ilionekana kuwa shughuli za uchimbaji mchanga,
ujenzi kando kando ya mto kuchangia kubomoka kwa kingo za mto, utupaji wa taka
ngumu(mto kutumika kama dampo) na utiririshwaji wa maji taka kutoka nyumba
zilizo jirani ya mto.
Hatimaye washiriki walipatiwa vyeti vya ushiriki na kuwa mabalozi wa Kampeni hii katika mikoa mingine: Mbeya, Arusha, Mwanza na Tanga.
Ratiba ijayo:
Arusha-Agosti 2016
Mwanza-Octoba 2016
Tanga-December 2016.
Matukio katika picha: Mto Mbezi, Dar es salaam
Picha na Jielimishe Kwanza Blog
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza Blog
"Kampeni hii ni endelevu, inahitaji msaada wa kifedha na ushiriki wa mashirika mengine zaidi.Unakaribishwa sana kuchangia au kujiunga nasi"
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni