Nimeamua kutumia maneno haya makali kutoka
kwa mwandishi Stephen R.Covey katika kitabu chake “The 8th Habits of highly effective people”
ili kukumbushana kuhusu masuala muhimu katika elimu na utendaji.
Picha kutoka:www.vpi-inc.com |
Nikizingatia mfumo mzima wa elimu, ambao umetuandaa
kuwa waajiriwa na si kutumia ufahamu na ujuzi tuliosomea kujiajiri na ikiwezekana kuajiri wengine ni muhimu sana kutafakari na kuwa na mtazamo mwingine.
Utakubaliana na mimi kuwa wafanyakazi wengi
nchini Tanzania wanafanya kazi nje ya taaluma zao.Lengo kubwa hapa ni kuangalia
maslahi, wakati huo huo wakiweka pembeni ubora na tija katika utendaji. Hapa
tunapata tatizo la kushuka kwa ubora wa huduma mbali mbali, hivyo kushusha
pato la Taifa.
Imezoeleka kuwa, ili mtumishi apande cheo au
kupanda ngazi ya mshahara, ni lazima aende kusoma zaidi.Swali la kujiuliza, je
wanachoenda kukisomea wanakitumia kuboresha utendaji?...jibu unalo msomaji.
Hapa nitarejea maneno yale yale…kujifunza bila kutenda ni sawa na kutojifunza
kabisa!
Kuna ugonjwa mkubwa sana katika Taifa hili, hasa kwa wafanyakazi au waajiriwa kupenda kufanya kazi kwa mazoea na si kutumia taaluma.Wengine wamebaki kunung'unika bila ya kuchukua hatua kwa kufuata utaratibu unaostahili.
Kuna tatizo jingine, hasa kwa wahitimu kutoka
vyuoni, utamwona “graduate” anajitamba na vyeti vyake kuwa anafahamu mambo
mengi kuhusiana na taaluma yake.Lakini tukimwambia onyesha uwezo wako katika
utendaji…mh! Ni shida kubwa.
Ningependa kuwafumbua macho vijana wengi waliomaliza
vyuo.Katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya uchumi yanayochochewa na
Sayansi na Teknolojia ni muhimu kuwa mtendaji na si mtu wa kufahamu peke yake.
Kama
malengo yako ni kuajiriwa basi tambua kuwa unatakiwa kuwa mchangiaji wa ubora
katika kampuni au sekta fulani. Ukikosa kuwa na mchango wa ubora katika kampuni
au sekta hiyo basi ujue utakosa kazi au kupewa ujira usiolingana na ndoto zako.
Mwandishi na msemaji maarufu wa hadhira-Jim
Rohn aliwahi kusema “people get paid by
bringing value to the market place” akimaanisha, “watu hulipwa ujira kulingana
na ubora wa kazi waletao kwenye soko, tunapozungumzia soko inamaanisha uhitaji
katika jamii.
Naomba nikuache na usemi kutoka kwa Raisi wa 26 wa Marekani Theodore Roosevelt alisema:
"Great thoughts speak only to the thoughtful mind, but great actions speak
to all mankind."-Mawazo makuu au fikra kubwa hueleweka kwa walio na upeo wa kufikiri, bali matendo makuu hueleweka kwa kila binadamu"
Imeandaliwa na Henry Kazula,
Jielimishe Kwanza!