PICHA:Yuichiro Miura,(80):www.outsideonline.com |
Mlima Everest, urefu mita 8,848:Picha imetolewa: www.guardian.co.uk |
Mpandaji milima Yuichiro Miura, 80, amefanikiwa kufika kilele cha mlima Everest
[Mei 23 2013], na kuwa mzee kikongwe wa kwanza duniani kupanda mlima huo mrefu kuliko yote duniani.Hili ni jaribio lake la tatu la kukwea mlima huo, jaribio hilo lenye mafanikio kwake lilihitaji uvumilivu na jitihada ya pekee,
bila kujali umri wake na uwezo wa afya yake aliamua kujitoa mhanga.
Akielezea changamoto alizopata katika kukwea mlima licha ya uzee wake,kikongwe huyo alisema, "ilikuwa ni changamoto ya aina yake kukifikia kilele cha mlima" "Imekuwa hivi kama heshima kubwa kwa asili ya Mama"alisema hayo kupitia mtandao wake"Akitumaini kuongeza hata chembe ya kuishi."
Miura hakufanikiwa katika jaribio lake la kwanza la kufika juu ya mlima Everest hadi mwaka 2003, akiwa na umri wa miaka 70. Alifanikiwa kutembea umbali mrefu akiwa na mtoto wake, na kujiwekea rekodi ya mtu mzee duniani kupanda mlima.
Habari hii ya kikongwe Miura iwe funzo kwetu tulio na nguvu na damu yenye kuchemka.Vipi tumejiwekea malengo? je kuna jitihada yoyote tunayofanya kuyafikia malengo? au tunabaki kila siku kusema"One day yes! au Kama Mungu akipenda..." na hali tukiwa tumebweteka na vile vidogo
tulivyo navyo?
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
I found this post incredibly insightful! I’ve been writing about Satpura National Park on my profile, and I’d love to connect with others interested in this topic. Feel free to visit my profile for more!
JibuFuta