Picha:www.edudemic.com |
Ukifuatilia kwa kina utagundua kuwa watu wengi wanapoteza muda na fursa njeti ya kutangaza shughuli au biashara wanazofanya.
Unajua ni kwa jinsi gani ilivyo rahisi kwa sasa kukutana na watu wengi unaowafahamu na usiowafahamu kupitia mitandao ya kijamii? Hivyo basi, tumia fursa hii kutangaza biashara yako au kazi unazofanya kwa huo umati wa wanajamii. Zingatia maadili na sheria za nchi unapotangaza biashara yako...
Kizuri zaidi hapa, hakuna gharama kubwa ya kujitangaza...ni bure kabisa! Ikiwa unahitaji kutengeneza ukurasa ili uwekwe kwenye upande wa matangazo ndiyo utalipia gharama kidogo kwa mtandao wa kijamii husika.
Naomba nikuhakikishie kuwa kwa kipindi hiki cha maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia ni rahisi mno kuwasiliana na watu wengi kuliko kawaida.
Imekuwa ni mazoea mtu kuweka picha mbali mbali mfano akiwa anakula, na nyinginezo za kujionyesha ili watu wabonyeze kitufe cha "like". Je, unaingiza shilingi ngapi kwa watu kubonyeza kitufe cha "like"? au unalipwa shilingi ngapi kwa kubonyeza kitufe cha "like"?
Kuna wengine kazi yao kubwa ni kubonyeza tu kitufe cha "like" hata kama kuna picha ya msiba au majonzi au kama kuna picha ya tukio la maovu.
Nisieleweke vibaya, namaanisha ni vizuri pia kuangalia faida ya mitandao hii ya kijamii kwa upande mwingine tofauti...hatimaye kujiongezea kipato.
Haya tuachane na hilo, tufanye nini ili kutengeneza pesa kupitia facebook,twitter, na mingineyo?
- Wajulishe marafiki kuhusu biashara yako, weka picha ya bidhaa unazouza na mawasiliano.
- Tumia muda vizuri kwa kuhakikisha "unachat" na mtu bila kusahau kumueleza biashara yako.
- Tengeneza ukurasa unaoeleza biashara yako, ukiweza ilipie ili ikae upande wa matangazo kutegemeana na mtandao wa kijamii husika
- Kwa wale wanaotafuta kazi, weka sifa ulizo nazo watu wajue uwezo wako...kwa hakika utajikuta unaunganishwa kupata kazi.Usione aibu kujielezea kuwa huna kazi.
- Tumia mitandao ya kijamii kupata fursa za kubuni aina ya biashara au huduma kwa jamii.
Kila la heri.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
i'm hero from arusha tanzania i need to creat my blog,
JibuFuta