Jarida maarufu la habari nchini Marekani-“Fox News” la tarehe
20 Mei 2013 limeripoti kuwa raisi wa Marekani-Barack Obama anataraji kuzitembelea nchi za kusini mwa jangwa la Sahara. Ziara hiyo muhimu itahusisha nchi tatu za Afrika; Afrika Kusini, Senegali na Tanzania.
Picha::www.letemps.blogs.com |
Taarifa kutoka Ikulu ya Marekani “White House” inasema kuwa
raisi Obama na mkewe Michelle Obama wataondoka Marekani tarehe 26 Juni 2013 kuelekea
Senegali, Afrika kusini na mwisho Tanzania.
Obama anatarajia kuonana na viongozi wakubwa wa nchi hizo,
ikiwemo viongozi wa makampuni ya biashara, mashirika ya kijamii na jumuiya
mbali mbali za vijana.
Utawala
wa “White House” umeeleza kuwa ziara hii ya Obama ni chachu ya mahusiano muhimu na yenye ukaribu kati ya Marekani na nchi za kusini mwa jangwa
la Sahara.
__________________________________________________________________
Sambamba na ujio huu mzito kwa Tanzania,Afrika Kusini na Senegali kumekuwa na manung'uniko mbali mbali hasa kwa nchi za jirani na Tanzania, eti kuwa -kwanini Tanzania? Ndugu msomaji naomba nawe ujiulize ni kwa nini? kwa nini si Kenya au Uganda au Rwanda au Burundi?
SOMA ZAIDI:
SOMA ZAIDI:
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni