Suala zima la kutunza muda ni muhimu sana
katika utendaji wa kazi za kila siku.
Wafanyakazi wengi na jamii kwa ujumla
wamekuwa wakitoa kipaumbele hafifu kwenye suala la utunzaji wa muda.Ni jambo la
kawaida sana kwa Watanzania na jamii nyingine za Kiafrika kudharau umuhimu wa
kutunza muda.Hapa unakuja ule usemi usemao;
“There
is no hurry in Africa” yaani hakuna haraka ukiwa Afrika.Pia baadhi ya methali
zetu zimetafsiriwa vibaya na wanajamii. Mfano: Pole pole ndiyo mwendo, Haraka
haraka haina baraka,Mwenda pole hajikwai na nyingine zinazofanana na hizi.
Itambulike
kuwa muda ni rasilimali inayoweza kumpa mtu mafanikio kama tu kutakuwa na
mipango inayoeleweka ikiwa sambamba na kujali muda.
Kwa
kipindi kirefu kumekuwa na taarifa mbali mbali kuhusu kuwepo kwa tatizo la msongo
wa mawazo au kwa lugha ya Kiingereza “Stress”.
Nikirejea,
maana halisi ya msongo wa mawazo-“Stress” iliyotolewa na Profesa Selye kutoka Chuo kikuu cha
Montreal nchini Canada alisema;
msongo wa mawazo au "Stress" ni muitikio wa mahitaji mbali mbali ya nje unaotokea
ndani ya mtu.Kwa maneno mengine, ni kitu kinachotuogopesha, au ni muitikio wa
mwili kwa vitu vinavyotuletea msongo wa mawazo-“Stressors” ambavyo mwisho wa
siku hutuletea hofu.Maana hii ya msongo wa mawazo imedumu tangu katikati ya
mwaka 1970 hadi leo ingawaje wanasaikolojia wamejaribu kuipinga bila mafanikio.
Wafanyakazi wengi na wanajamii wengine wamekuwa
na tatizo la msongo wa mawazo-"Stress" linaloambatana na suala zima la utunzaji wa muda, ingawaje wamelifanya tatizo hili kuwa la kawaida ilihali wakijua linaweza
kuwapelekea kupata magonjwa kama vidonda vya tumbo na shinikizo la damu.
Chanzo
cha msongo wa mawazo kama alivyoainisha Graham Jones katika kitabu chake cha "Fit To Manage" anasema; Mara zote msongo wa mawazo unachangiwa sana
na watu “kutokujua wanakoenda- ”pia tabia ya mtu kutotabirika.
Kukosa muelekeo wa maisha ya kila siku ni tatizo kubwa.Ni kitu cha kustaajabisha kumuona mtu akiwa hana utaratibu wa siku, yaani yupo yupo tu...kwa lugha nyingine ni kuwa hana malengo na maisha yake.
Swali la msingi hapa, ni kwa vipi kutunza muda
kunaweza kupunguza au kuepusha tatizo la msongo wa mawazo?
Kuna njia takribani 10 za matumizi sahihi ya muda zinazokuwezesha kuepukana na msongo wa mawazo hasa katika mazingira ya kazi:
1.WEKA
MPANGO WA SIKU
2.JIWEKEE
VIPAUMBELE VYA SHUGHULI ZAKO
3.SEMA
HAPANA KWA SHUGHULI ZISIZO MUHUMU
4. CHUKUA
MUDA KUFANYA KAZI YENYE UBORA
5. RAHISISHA
KAZI NGUMU, ZENYE KUTUMIA MUDA MREFU KULINGANA NA UWEZO WAKO
6. JARIBU
KUTUMIA KANUNI YA DAKIKA 10-GAWA SHUGHULI ZAKO KWA MUDA WA DK 10
7. JIPIME
JINSI UNAVYOTUMIA MUDA WAKO
8. EPUKANA
NA VITU VINAVYOKUHARIBIA KAZI, MFANO KUANGALIA TV UKIWA UNAFANYA KAZI
9. PATA
MUDA WA MAPUMZIKO, KULA VIZURI, FANYA MAZOEZI
Graham Jones .(1988).Fit To Manage. An Executive Fitness Guide To Peak Performance. England: Thorsons Publishing Group, Wellingborough, Northamptonshire
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni