Picha na www.wisegeek.org |
Utafiti wao
uliowahusisha wanaume 27,000 wenye umri kati ya miaka 45-82 ulionyesha kuwa
wale wasiokula kiamsha kinywa wako katika hatari ya matatizo ya moyo. Wakati wa
utafiti huo, zaidi ya watu 1,500 waliathirika kutokana na mshtuko wa moyo.
Utafiti huo ulithibitisha kuwa watu
waliokosa kifungua kinywa wako katika hatari kubwa ya kupata matatizo ya moyo
kwa asilimia 27 kuliko wale wanaokula asubuhi.
Ukizingatia
utafiti uliofanywa na Chuo kikuu cha Harvad kitivo cha afya ya jamii
kilisema kuwa: “kukosa kiamsha kinywa
kunasababisha mwili kutumia nguvu nyingi zaidi kuliko kawaida.” Sambamba na
utafiti huo, taasisi ya matibabu ya moyo nchini Uingereza imebaini
kuwa “kiamsha kinywa huwazuia watu kula vitu vyenye sukari kabla ya
chakula cha mchana.”(http://www.bbc.co.uk/swahili/kwa_kina/2013/07/130723_kiamsha_kinywa.shtml).
Kupata kifungua kinywa kwa mtu wa kipato cha chini inawezekana...si lazima iwe kama picha inavyoonyesha, ni muhimu kuzingatia makundi ya vyakula unayotakiwa kula kulingana na kipato chako.Yote tisa, kifungua kinywa ni muhimu sana kwa afya yako.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!