-->
Picha na www.pbs.org |
Mzazi/Mlezi
unaonekana kama kioo kwa mtoto.Mtoto anajifunza mengi kupitia wewe, pia
anaamini mafundisho yako.
Tukizungumzia utamaduni wa kusoma vitabu vyenye tija
ya kuelimisha, ni muhimu sana kumjenga mtoto wako akiwa katika umri unaoendana na hatua ya kutaka kujua
mambo mengi- hasa kwa kukuuliza maswali mbali mbalimbali.Toa majibu mazuri kwa mtoto ukiambatanisha na maarifa kutoka kwenye vitabu.
Kwa sasa najua sio
tatizo tena kwa mzazi kusoma kitabu chenye tija ya maendeleo, hasa ukizingatia
somo lilitolewa kupia makala ihusuyo mbinu 10 za kuanza kusoma kitabu chenye tija
ya maendeleo kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html?utm_source=BP_recent
Leo naomba ufuate
nami katika hatua nyingine ya ujasiri na yenye mafanikio katika kumjengea mtoto wako uwezo
na shauku ya kuwa msomaji wa vitabu.
1.
Kuwa mfano wa kuigwa katika kusoma kitabu…weka
utaratibu unaoleweka na kufuatwa na familia kuhusu usomaji (najua hili sio
tatizo tena kwa kuwa umesoma na kuzifanyia kazi mbinu 10 kupitia http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/elimu-na-mtazamo-mbinu-10-za-kuanza.html?utm_source=BP_recent
2.
Msomee mtoto wako kitabu na kumsaidia sehemu
zenye utata (Zingatia umri na uelewa wa mtoto)
Picha na home-startwigtownshire.co.uk |
3.
Mwekee mtoto utaratibu wa kusoma kitabu na
kuwasilisha taarifa fupi mara amalizapo sehemu ya kitabu au kitabu chote…soma zaidi http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/07/malezi-na-elimu-ukitaka-mtoto-wako.html (Zingatia
umri na uelewa wa mtoto)
4.
Jenga utamaduni wa kununua vitabu mbali mbali
vyenye kuchochea maarifa kwako na kwa mtoto( unaweza kuweka utaratibu wa
kununua vitabu 3-5 kwa mwezi)
5.
Mpongeze mtoto anapoonyesha juhudi ya kusoma
kitabu-chagua zawadi zinazochochea usomaji zaidi mfano kumpeleka sehemu tulivu
ya kuvutia ili kujisomea na kuburudika.(Zingatia hali ya kipato chako-huna sababu ya kujitetea, zipo sehemu nzuri za mapumziko zisizohitaji hata pesa)
Hongera
sana kwa kutimiza zoezi hili!
Maarifa mengi sana
yamefichwa kwenye vitabu…
Yapekue!
Yasome!Yaelewe!Yafanyie kazi kwa dhati hasa yale yanayofaa kwa wakati husika.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Ikiwa una maoni au una hitaji ushauri kuhusu usomaji wa vitabu
ulio na manufaa,usisite kuwasiliana nasi. Hakuna gharama ya huduma hii!
0785 175 157 Barua
pepe:jielimishekwanza@gmail.com