-->
Mzazi
au mlezi una mchango mkubwa kumfanya mtoto wako awe kinara katika mitihani
mbali mbali inayotolewa shuleni.
Tukiondoa
juhudi za walimu, uwezo wa mtoto kitaaluma huanza kujengwa kuanzia nyumbani
hasa katika ngazi ya chini kabisa kwa kumuandaa mtoto kupenda kujisomea.
Wakati
huo huo mzazi unatakiwa kuweka mkazo juu ya zoezi zima la kujisomea na
kulifanya kuwa ni sehemu ya utaratibu wa kila siku nyumbani. Hii haijalishi
kama hukusoma, ila jitahidi kulisimamia zoezi hili kikamilifu ukijifunza kwa
wazazi wengine waliosoma.
Sambamba
na zoezi hilo unatakiwa kufanya hivi:
1.
Mpangie utaratibu wa kusoma kitabu kimoja na kuwasilisha taarifa ya maandishi
na atoe maelezo yake mwisho wa wiki.
2.Mfanye
mtoto ajitambue kuwa anaweza kujiongoza.Pia tambua na thamini uwezo wake.Hii
itamuongezea hali kujiamini na kumjengea hali ya uthubutu wenye tija.
3.Mpongeze
mwanao anapoonyesha mafanikio au kubadilika tabia.Unaweza kutoa zawadi zinaweza
kuchochea tabia njema kulingana na uwezo wako kifedha.Hakikisha kuwa zawadi
unayotoa isiwe tafsili kuwa amefanya vizuri kukufurahisha mzazi ila imjenge
kuwa ni kwa manufaa yake.
4.Shirikiana
bega kwa bega na walimu kwa kujua maendeleo ya mtoto wako kitaaluma. Hili si la
kupuuza hata kidogo! Usishirikiane na mtoto wako kumshambulia mwalimu…
shirikiana na mwalimu kumuongoza mtoto wako katika njia ifaayo.
5.Kemea
tabia ya kuangalia Televisheni, filamu na intaneti kwa mambo yasimjenga
kitaaluma.Hamasisha kuangalia vipindi vya kitaaluma.
Kuna mbinu nyingine nyingi zilizo halali unazoweza kufanya kumsaidia mtoto wako kufaulu mitihani yake.
Tuwasiliane, tutajulishana.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni