Shirika
lisilo la kiserikali “Youth for Africa (YOA)” kwa kushirikaiana na TCRA,uhuruone,Clouds
FM,Bongo 5,Caravan Records,KINU,onspot magazine,Coca Cola Hussein, Africa
2.0 limezindua zoezi la kutunuku tuzo
maalum zijulikanazo kwa lugha ya Kiingereza “Under
-30 YOUTH AWARDS 2013” ikiwa ni mwanzo tu wa tukio hilo kubwa linayotarajiwa kufanyika tarehe 17/08/2013.
Tuzo
zimeandaliwa rasmi kwa vijana waliothubutu na kufanya vizuri katika nyanja za
ujasiriamali, Uandishi wa habari, mchango kwa jamii, Sanaa na Ubunifu, Mitindo,Muziki
na Burudani, Uvumbuzi na Michezo.
Uzinduzi huo
ulishirikisha wadau mbali mbali wa masuala ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano uliongozwa na mgeni rasmi Mhe.January Makamba(MB).
Mhe.Makamba alisisitiza kuwa ni vyema YOA na wadhamini wa tuzo hizo kuweka utaratibu wa kuwatambua vijana ambao hawahamiki na wanafanya vizuri katika nyanja mbali mbali za ubunifu na ujasiriamali na kuwafikia mahali popote nchini Tanzania.
Mhe.January Makamba(MB) akizindua rasmi zoezi la utoaji tuzo kwa vijana wenye umri chini ya | miaka 30. |
Shughuli nzima ya kuwapata washindi wa tuzo itahusisha wanajamii wote kwa kupiga kura kwa mshiriki husika kupitia ujumbe mfupi wa simu ya mkononi kwa kuandika YOA kwenda namba 15584...ujumbe huo mfupi utatozwa Tsh. 200.
PICHA: UTOLEWAJI WA VYETI KWA WASHINDANI WA TUZO
Wakiwa katika nyuso za furaha ni washindani wa tuzo wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe.January Makamba (MB). |
Wadhamini wa tuzo "Under 30 Youth Awards 2013" wakiwa na Mhe.January Makamba |
Jopo zima la YOA wakiwa na Mhe.January Makamba(MB) |
Tushirikiane kwa pamoja kufanikisha zoezi hili ili iwe chachu ya mabadiliko ya kiuchumi yaliyo na tija kwa vijana na Taifa kwa ujumla.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni