Picha na www.techtricksworld.com |
Nikirejea makala iliyopita kuhusu elimu na
utendaji: http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/05/elimu-na-utendaji.html niligusia suala la kufanya kazi nje ya taaluma mtu aliyosomea kutokana na uhaba
wa ajira, hivyo mtu kujikuta anafanya kazi yoyote bora mradi kujipatia mkate wa
kila siku.
Picha na www.secrets-2-success.com |
Kiuhalisia watu wanafanya kazi nje ya kile
walichokisomea na nje ya dhamiri (passion) zao, hivyo hufanya kazi bora
mradi tu wapate kipato.
Ndani ya mioyo yao wana ndoto kubwa zinazowajia kila siku, zilizo sanjari na vipaji vyao, pia wakiwa na shauku kubwa ya kuzitimiza ndoto hizo lakini majukumu ya kazi yanawabana kiasi kwamba wanashindwa kutimiza ndoto zao.
Ndani ya mioyo yao wana ndoto kubwa zinazowajia kila siku, zilizo sanjari na vipaji vyao, pia wakiwa na shauku kubwa ya kuzitimiza ndoto hizo lakini majukumu ya kazi yanawabana kiasi kwamba wanashindwa kutimiza ndoto zao.
Je, wewe pia upo katika kundi la watu
wanaotaka kuwafurahisha mabosi wao kwa kufanya kazi kwa bidii bora mradi wapate
mkate wao wa kila siku? Au upo kwenye kundi la wale wanaosema;
·
“yaani hii kazi…mh! Nafanyia shida tu!”
·
“nafanya kazi bora mradi mkono uende kinywani”
·
nafanya kazi hii kwa sababu mzazi wangu amesema
niifanye…lakini siipendi”
·
nafanya kazi hii kwa sababu ajira ni ngumu
sana…ila nasogeza siku tu!
Huna sababu ya kunung’unika…fuata dhamiri yako na kile moyo
unapenda kwa sababu utakifanya kwa ufanisi, ukiwa huru, pia kutimiza malengo
yako na ya wengine.Kama Steve Jobs- mjasiriamali, mwanzilishi na mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya "Apple Computers na Pixar Animation"
alivyosema; Have the courage to follow
your heart and intuition.They somehow already know what you truly want to
become.Everything else is secondary”.
Kama wewe ni miongoni
mwa watu (wafanyakazi) wanaofanya kazi kwa manung’uniko tajwa na una lengo la
kufanya kile ukipendacho na kutimiza ndoto na dhamiri yako fanya yafuatayo:
1. Andika ndoto yako kwa
maandishi mfano unaweza kuiweka katika mpango wa biashara
2. Jichunguze mbinu
ulizonazo kufikia ndoto yako…unaweza kuongeza ujuzi kwa kusoma vitabu husika,
pia kupitia mtandao wa internet (muulize mwalimu Google) atakuelekeza au fanya
utafiti wa biashara yako
3. Tenga muda japo masaa
mawili ya kufanyia kazi ndoto yako
4. Jibidishe mwenyewe
zaidi kuliko unavyojibidisha kwa bosi wako-Jim Rohn.Jiwekee utaratibu wa kujifunza kwa hali na mali.
5. Tumia sehemu ya
kipato unachopata kuweka msingi wa biashara yako
“Mfumo usikuzuie kutimiza ndoto yako, unaweza timiza ndoto
yako nje ya mfumo”
Kwa ushauri zaidi,
tuwasiliane.
Huduma ya ushauri ni
bure!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni