inspire

inspire

Lebo

AFYA (8) AJIRA (5) BIASHARA (39) ELIMU (14) MAHUSIANO (2) MALEZI (16) MAZINGIRA (12) SAIKOLOJIA (48) VIJANA (7)

Business registration

Green Consulting

business consultancy

business consultancy

Business consulting-2

Business consulting-2

Professional Consulting

PDC

Swahili translator

Swahili translator

TANGAZO-KITABU

E-BOOK: MTAZAMO WAKO NI UPI?

TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- .... TANGAZO:Kitabu kipya. Kitabu! Kitabu!Kinauzwa Katika Maduka Ya Vitabu.Pia M-Pesa 0754 572 143, Tigo Pesa 0716 075 826.Ili Kikufikie Ulipo, Tafadhali Ongezea Sh.10,000/- ....

TANGAZO TUWEZESHANE

TANGAZO TUWEZESHANE

DARDY'S INVST-20/10/2017

DUNIA IKUONE

DUNIA IKUONE

Alhamisi, 8 Agosti 2013

ELIMU NA MTAZAMO: NINI HATMA YA KIWANGO CHA ELIMU ULICHONACHO…JE, KIMEKUPA FURAHA YA MAISHA?

-->

Picha na successfulworkplace.com


Ni dhahiri na ukweli usiopingika kuwa watu wengi wanaamini kuwa ni elimu pekee ndiyo mkombozi na chanzo cha furaha maishani.Ikiwa ni sanjari na msemo wa Kiswahili usemao; “Elimu ni ufunguo wa maisha” yaani bila elimu hujafungua maisha au …! Bila shaka unakubaliana na dhana hii.

Wanafunzi kuanzia ngazi ya awali hadi chuo kikuu wanasoma sana na hatimaye wanapofika mwisho wa safari yao huanza  kulinganisha walichojifunza na maisha halisi na mwisho wa siku tunajikuta tuna makundi tofauti tofauti yenye mtazamo tofauti tofauti kwa mfumo ule ule wa elimu:
·      Wengine huona kama wamepotea njia,

·      Wengine huanza kushtuka kuanza kuchagua kitu cha kufanya wakiwa wamehitimu

·      Wengine hujitamba kuwa wana vyeti vizuri na kujitukuza…hivyo kuchagua aina ya kazi

·      Wengine huanza kutumia kile walichosomea kutatua matatizo katika jamii kiuhalisia

·   Wengine hufurahia kutumia walichosomea kupanda vyeo sambamba na ngazi za mshahara

·      Wengine hutumia elimu ndogo waliyo nayo kupewa kazi wasizoweza kuzimudu

·      Wengine, wamethubutu kuviongezea vyeti vyao uwezo kwa kuambatanisha na vya watu wengine kupata ajira zinazofahamika kuwa na maslahi

…ndiyo hivyo, utaamua mwenyewe kujiweka kwenye kundi ulipendalo!

Swali la msingi

Naomba ujiulize, unakitumia kile ulichokisomea kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu? au ilikuwa ni kwa ajili ya kupata cheti tu au heshima isiyo na faida?

Hivi ina faida gani kusomea taaluma fulani kwa miaka 3 au 4 au 5 halafu isitumike kuboresha utendaji au kutatua matatizo katika jamii? Kwa mtazamo mwingine ni sawa na kupoteza muda na rasimali pesa ya Taifa.

Hivi tukitafakari kwa kina, nini lengo kuu la elimu? Ninaweza kuanisha malengo kadhaa ya elimu

·      Kuchochea na kukuza vipaji…elimu inapaswa kuchochea/kukuza vipaji na si kudumaza vipaji

·      Kuboresha mtazamo wa kufikiri na kutenda hasa katika kutatua matatizo ndani ya jamii

·  Kumpa mtu ujuzi wa kufanya kazi kutegemeana na kipaji chake…je unafanya kazi kulingana na kipaji chako?…au bora mkono uende kinywani?

·      Kujenga mahusiano mema, ushirikiano na watu wa jamii tofauti tofauti

·      Kumkomboa mtu na utumwa wa fikra…kumfanya mtu kuwa huru kifikra



Nini tufanye ili kuitendea haki elimu tuipatayo shuleni kwa manufaa ya jamii nzima hasa ile iliyokosa fursa adimu ya kupata elimu?

Kuna manung’uniko kila kukicha kuhusu ukosefu wa ajira…lawama zote hutupiwa serikali…hivi serikali ni nani? Bila shaka utajibu kuwa ni watu, na watu wenyewe ni kama wewe na mimi!

 Inasemekana, serikali pekee ndiyo yenye jukumu la kutengeneza ajira.Sasa umefika wakati kwa wahitimu wa vyuo vikuu na wanajamii kwa ujumla kutengeneza ajira na si kuitegemea serikali pekee…nikuahakikishie hata ungekuwa wewe madarakani usingefanikiwa kumpatia kila raia ajira anayoitaka kwa wakati anaotaka!

Tunapaswa kutumia tulichokisomea na vipaji vyetu kutatua matatizo katika jamii kwa kuongeza fursa za ajira kwa wengine.

Nikimnukuu Hayati baba wa Taifa Mwl.J.K.Nyerere aliwahi kuweka msisitizo “Haitoshi kusema nafahamu, kufahamu kunapaswa kubadilishwa kuwa nyenzo katika kuboresha maendeleo ya jamii”

Pia unaweza kusoma makala hii muhimu inayoendana ELIMU NA UTENDAJI: KUFAHAMU BILA YA KUTENDA NI SAWA NA KUTOFAHAMU KABISA!KUJIFUNZA BILA YA KUTENDA NI SAWA NA KUTOJIFUNZA KABISA! kwa kubofya http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/05/elimu-na-utendaji.html

Education is what remains after one has forgotten what one has learned in school. Albert Einstein 
Education is not the learning of facts, but the training of mind to think -Albert Einstein

Huu ni mtazamo tu wa Jielimishe Kwanza!
Ikiwa una maoni au ushauri,

Usisite kutuandikia kupitia: