Kila mtu ana mazoea ya jambo fulani, hasa
baya kwa kufahamu au kutokufahamu.Kuna aina tofauti tofauti za mazoea mabaya. Leo napenda nikujuze aina zifuatazo za mazoea mabaya na mbinu za kuondokana tatizo hilo;
Watu wengi wamejikuta tu wameingia kwenye
mkumbo wa kutumia vitu mbali mbali kama ulevi, uvutaji sigara na pia madawa ya
kulevya kutokana na ushawishi wa marafiki na watu wa karibu.Bila shaka kila mtu
anajua ni jinsi gani alivyoshawishika kuingia katika mkumbo huo na mwisho wa
siku kujikuta ni mzoefu aliyebobea katika utumiaji wa vitu hivyo vibaya.
Kama msemo maarufu wa
Kiswahili usemao “mazoea hujenga tabia” hivyo basi mazoea mabaya hujenga tabia
mbaya.
Tunaondoka
vipi hapo tulipo?
Picha na editionstv.com |
Jielimishe Kwanza! imewahi kufanya mahojiano
mbali mbali na watumiaji wa muda mrefu wa sigara,pombe na wengine wenye tabia zinazofanana na hizo kuhusu
utaratibu wa kuacha, wengi wao walisema wanataka kuacha ila hawawezi.
Leo naomba nikujuze mbinu mbadala za
kuondokana na mazoea mabaya:
1. Anza
leo/sasa kujizuia kutumia vitu vibaya...ukihisi hamu ya kutumia vitu hivyo vibaya, tumia chakula,matunda au kinywaji kisichokuletea tatizo kama la awali (Taadhari! Anza kuacha kwa kupunguza idadi ya matumizi)
2. Jenga
uhusiano mwema na Mungu wako kwa kufuata amri zake
3. Epuka
makundi au marafiki wabaya
4. Jaribu
kushirikiana na watu waliofanikiwa kuacha matumizi ya vitu vibaya
5. Tumia
watu wenye tabia njema kukumbusha pale unapotaka kurudia mazoea mabaya
Tuungane kipindi kingine tujuzane kuhusu mbinu za kupambana na zoea jingine la
"ULAJI MBAYA" ambalo kwa sasa limekuwa ni tishio kwa afya za watu wengi duniani.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!