Kwa kipindi kirefu mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro
umekuwa kinara wa kudumisha usafi wa mji na makazi ikiwa ni sambamba na kujizolea tuzo za kutunza mazingira nchini na Kimataifa.
Kutokana na utafiti
uliofanywa na Jielimishe Kwanza! umebaini siri ya mafanikio ya mji huo ili iwe
mfano wa kuigwa kwa miji mingine nchini.Hii ndiyo siri;
Usimizi wa Dhati
wa Sera na Sheria za mazingira
Kama ilivyoanishwa katika Sera ya Taifa ya mazingira ya
1997 ambayo inasisitiza umuhimu wa kutunga sheria za mazingira na sheria za
Sekta hiyo, kitu ambacho ni cha lazima katika kusimamia ipasavyo usafi mazingira na kustawisha uhai.
Sheria za mazingira zinazofaa na zenye maana ni lazima
zieleweke sawa sawa na kuthaminiwa na jumuiya na watu wanaolengwa.
(Ukitaka kujua Sera ya Taifa ya mazingira ya 1997 soma
kupitia NEMC.
Ni jambo linaloeleweka na kila mtu mjini Moshi kuwa
hutakiwi kutupa taka ovyo, kukojoa ovyo kutema mate,au makohozi hadharani.Kinyume na hapo ni
kutozwa faini isiyopungua Shilingi Elfu hamsini (50,000/=) na hili limesimamiwa kikamilifu.
Huu ni uthibitisho wa mahojiano mengine ya tarehe 24 Juni 2013 yaliyofanywa na http://www.ippmedia.com/frontend/?l=56280
pamoja na Afisa wa Afya wa
Manispaa ya Moshi, David Kimaro ambaye alisema;
sheria hiyo inasaidia halmashauri kupata mapato yatokanayo na faini kwa wanaochafua mazingira kupitia kampuni tatu za uwakala ambazo zinakusanya Sh, milioni 14.4 kwa mwaka.
Kampuni hizo kwa kutumia sheria ya usafi wa mazingira kumtoza faini ya Sh. 50,000 mtu yeyote anayekojoa hovyo, kutema mate, kutupa taka kama chupa za maji, magunzi, vichungi, sigara, maganda ya ndizi, vocha za simu ama kutiririsha maji.
Wageni wa mji huo ukijumuisha watalii wanajulishwa
mapema kuhusu suala zima la usafi…tembelea vituo mbali mbali vya kusafirisha
watalii utaona tangazo linalohusiana na Sheria hii kali kuhusu utunzaji wa
mazingira.
Hivyo jihadhali uingiapo mjini Moshi.Pia huu uwe mfano wa kuigwa nchini kote, kama limewezekana Moshi kwanini iwe shida mikoa mingine nchini?
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!