Kumekuwepo na changamoto nyingi kwa
wafanyabiashara wadogo pia hata wale wanaolekea kuwa na biashara kubwa.Moja ya
changamoto kubwa kwa biashara ndogo na zilizoanza ni kushindwa kukuza soko la
biashara na faida ndogo iliyo tofauti na malengo ya mmliki/wamiliki wa biashara
fulani.Pia mitaji midogo ni changamoto nyingine inayodidimiza kupanuka kwa
biashara ndogo.
Tukitambua na kuzitumia changamoto zilizopo
kama sehemu ya kusimamia ni vyema tukashirikishana kwa pamoja mbinu 10 mbadala
za kuboresha biashara zetu kwa mafanikio tarajiwa kwa muda tuliojipangia.
1.ANDIKA NA UFUATE MPANGO WA BIASHARA “Business plan”
Ukiwa na wazo la biashara ni vyema ukafanya
upembuzi yakinifu kupitia mpango wako wa biashara.Kupitia mpango huo wa
biashara uliouandika utaweza kupunguza hatari zilizopo katika biashara yako,pia
utaona ni kwa njia ipi utapata faida na utajua muelekeo wa biashara yako kuliko
kuingia kichwa kichwa katika biashara.
2.PENDA KILE UNACHOKIFANYA, utakifanya kwa
bidii…Kama Steve Jobs- mjasiriamali, mwanzilishi na mkurugenzi
mtendaji wa Kampuni ya "Apple Computers na Pixar Animation"
alivyosema; “huna sababu ya kutofuata
ukipendacho” Hii ni muhimu sana kwa biashara changa.
3.IFANYE BIASHARA YAKO KUWA NA HUDUMA AU
BIDHAA ZA KIPEKEE
Kufanikisha hili fanya utafiti wa soko la
bidhaa na huduma za washindani wako, BORESHA! ukijitofautisha nao ila
ukihakikisha unakidhi mahitaji ya wateja wako.
4.HAKIKISHA UNAWASHIKA WATEJA WAKO…fanya hivi
ukichukulia kama wamekuja ofisini kwako kwa mara ya kwanza…usiwachukulie
kimazoea na kuwapuuza.Hili ni muhimu sana kwa wateja wa mwanzo kwa sababu
wanakwenda kukufanyia matangazo bila gharama yeyote.
5.TENGENEZA WIGO WA SOKO LAKO
Hakikisha unalenga wahusika wa aina fulani.Mfano.Kama
unauza nguo za jaribu kujitofautisha na wengine kwa kuzingatia rika na
jinsia.Hii itakusaidia kuitofautisha biashara yako na wengine hivyo kuwa na
wigo wa uhakika wa soko lako kibiashara.
6.JITENGENEZEE MTANDAO MZURI…zingatia
ushirikiano wa kibiashara wenye kufaidiana kibidhaa au kihuduma.Mfano kampuni
moja haiwezi kuwa na kila kitu, ni lazima itahitaji huduma au bidhaa kutoka
kampuni nyingine…hii nisehemu nzuri ya kutenga mtandao mzuri ukiwa makini
kuangalia fursa.
7.WEKA LENGO LA KUIFANYA BIASHARA YAKO KUKUA
IKIWA NA FAIDA ENDELEVU…
Tukizingatia ushauri wa
wafanyabiashara…inatambulika kuwabiashara imara na yenye tija ya faida endelevu
ni ile inayokuwa kulingana na muda na malengo ya kukua.Inatarajiwa kuwa
biashara iliyokuwa inahusisha kutembeza bidhaa inaweza kuonyesha hali ya kukua
hasa kwa kumiliki duka la bidhaa.
8.SOMA ALAMA ZA NYAKATI
Ni vyema kujua aina na wakati wanapopatika
wateja wako kulingana na aina ya bidhaa au huduma yako. Usifanye biashara
kimazoea ukiwa na lengo la kukuza biashara yako.Hakikisha unabadilika kulingana
na mazingira…na hii ni sifa mojawapo ya mjasiriamali.
9.THAMINI NGUVU YA TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
10.USIKATE TAMAA PALE UNAPOPATA HASARA...tumia mapungufu yako kujiboresha zaidi.
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!