Najua jinsi inavyouma au kukatisha tamaa
unapokuwa na wazo lako la biashara unaloliamini sana kukutoa kimaisha. Imezoeleka
sana kwa watu kupenda kuwashirikisha ndugu, marafiki au jamaa wa karibu malengo
yao ya biashara.Yafuatayo ni baadhi ya majibu wanayopata wajasiriamali wachanga
mara tu baada ya kueleza nia zao za kuanzisha biashara;
·
Mh! Yalimshinda…………utaweza wewe?
·
Hivi nani kakwambia biashara hiyo inalipa kwa
sasa!
·
Huogopi kupata hasara? Wengi sana wameporomoka
na hiyo biashara!
·
Hiyo biashara inahitaji mtaji mkubwa sana,
hakika hutaimudu!
·
Utapata wapi mtaji?
·
Hebu acha kupoteza muda wako…
Bila shaka maswali haya yanakatisha tamaa na
kukupa hasira.Naomba nikufumbue macho ndugu msomaji…hasira hiyo ndiyo inayokufanya
uboreshe sehemu zote zenye mapungufu katika wazo lako la biashara.
Hivyo, hupaswi kugombana wala kurumbana na
kundi hilo linalokupa changamoto.Suala la msingi ni kutulia, kushusha pumzi,
hasira zetu na kuwasikiliza kwa makini na kuwa wajanja kung’amua sehemu zenye
mapungufu na kuboresha.
Faida nyingine ya kundi hilo linalotoa
changamoto ni kukupa msukumo wa kusonga mbele na kukupa hasira ya kumiliki vitu
binafsi.
Jaribu kufanya utafiti mwenyewe utakubaliana nami na hata kuamua kunipigia
simu +255
754 572 143.
Ukiona watu wanakupongeza na kukubali kila
unachowaambia…kuna walakini!
“I like
oppositions and criticism ,they make me behave better with perfection-Henry
Kazula.
USIOGOPE VIKWAZO, KUPINGWA...CHUKULIA HALI HIYO KAMA SEHEMU YA KUJIJENGA ZAIDI, UKIBORESHA UTENDAJI WAKO!
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni