-->
Jielimishe Kwanza wanapoamua kukuelimisha
kuhusu uhuru hawamaanishi wa nchi au Taifa ila ni ule uhuru wa mtu binafsi.Hii
inamaanisha kuwa uhuru wa Taifa kwa ujumla wake unaanzia na mtu mmoja.
Picha na www.freedomideas.com |
Nikimnukuu Mkurugenzi wa Jielimishe
Kwanza! Henry Kazula katika moja ya mafunzo yake aliwahi kusema; "Mtu mmoja hawezi kuleta mabadiliko yote katika
dunia, lakini mabadiliko duniani huanzia na mtu mmoja".
Taifa linaweza kuwa huru lakini watu wake
wanaweza wasiwe huru kimtazamo, kiakili, kiuchumi na kifikra.
Ndugu msomaji najua kwa haraka haraka
unaweza usinielewe…soma makala hii ukiirudia tena.Naomba nikukumbushe moja
ya makala zetu inayoelezea na kutoa suluhisho la jinsi ya kuepukana na utumwa
wa kifikra http://jielimishekwanza.blogspot.com/2013/09/mtazamo-hivi-ndivyo-tunavyoweza.html
Pia nikulete moja kwa moja kwenye suala
la jinsi uhuru wako unavyoweza kutekwa na mtu mwingine bila wewe kujua.
Vifuatavyo ni baadhi ya viashiria vinavyozingatia mtazamo wa kisaikolojia;
- Kupewa vitu au fedha bure
- Kutumika kifedha na si fedha ikutumikie (working for money and not money working for you).
Hamasika!
Hamasisha Uhuru wa Kimtazamo, Kiakili, Kiuchumi na Kifikra.
Usikubali mtu
atawale Uhuru wako!
“I know but one freedom and that is the
freedom of the mind.” ~Antoine de Saint-Exupery
Imetolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni