Picha na blog.bounzd.com |
Kwa
kuzingatia maombi ya wasomaji wetu, tumeonelea ni vyema tukamalizia njia nyingine 3 zilizobaki za kupambana na kumshinda mshindani katika biashara, ikiwa wengi wamejaribu kuzitumia njia mbili zilizotolewa katika
makala iliyopita kwa mafanikio ya kuboresha ushindani wa biashara zao.
Nasi
bila hiyana leo tunamalizia njia hizo kama ifuatavyo;
3.Ongeza thamani ya ubora
Wafanyabishara
wengi hufikiri kuwa wakishusha bei zaidi ya mpinzani watalishinda soko,
La
hasha! Ikiwa mfanyabiashara kafikia hatua hii ujue kasahau kuwa, wateja hununua
thamani ya kitu kwa lugha ya
Kiingereza “value” ikiwa na maana ya
kumridhisha mteja na si gharama ya kitu.Chukulia mfano wa bidhaa na huduma za
Kampuni ya Apple zilivyo na thamani ya ubora inayoendana na gharama.
Ingekuwa
wateja wanaangalia gharama, hakika watu wachache sana wangeweza kumudu.Ila kwa
kuzingatia thamani ya ubora, watu wanajitahidi kumiliki bidhaa na huduma za
Kampuni ya Apple.
Hivyo,ongeza
thamani ya ubora ikiwa sanjari na ongezeko la bei zaidi ya mpinzani wako…Hakika
utalishinda soko!
4.Thamini kila mteja
Usijaribu
hata siku moja kumbeza mteja wa aina yeyote ile, huwezi kujua leo kanunua kitu
cha sh.1000 kesho atanunua kitu cha sh.10,000 nakuendela.Pia ujue kuwa wateja
wako wanachukua sehemu kubwa ya matangazo, tena wanakufanyia matangazo
bure! kwa njia ya mdomo…ni kwa sababu umewauzia thamani ya
ubora wa huduma na bidhaa.
Hii ni njia nzuri ya kucheza na saikolojia ya
wateja wako, wakati huo huo ukiendelea kumshinda mpinzani wako katika soko.
5.Weka motisha kwa mteja
Njia hii ni nzuri ikiwa unaifuata njia
namba 4.Njia hizi mbili zinaendana sana.Bila kujali aina ya mteja, hakikisha
unajua kwanza motisha zitolewazo na mpinzani/wapinzani wako.
Mifano tunayo
mingi, hebu jaribu kuchunguza makampuni ya simu jinsi yanavyocheza na akili za
wateja kwa kuweka vijimotisha kila kukicha.Lengo lao kubwa ni kuhakikisha
unabaki kwenye kampuni ya simu husika.Hata kama makampuni yote yanatoa motisha,
usihofu!…mteja ndiye mwenye chaguo, atahakikisha anapata motisha kutoka kila
kampuni kulingana na huduma itolewayo kwa wakati husika.Nawe hutakuwa na kitu cha kupoteza.
Mwisho, ndugu msomaji na mfanyabiashara nikutakie kila la heri katika kuboresha na kuimarisha biashara yako,
usije kulogwa kumchukia mpinzani wako, huyu anakusaidia sana kuboresha biashara
yako na kuifanya isibaki kama ilivyo kwa miaka nenda rudi.Hivyo mjue undani wake, Soma na boresha thamani ya ubora.
Kwa ushauri na maelekezo ya biashara, usisite kuwasiliana nasi,
+255 754 572 143
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni