M
|
ara nyingi hupendelea kusoma magazeti ya ndani na nje ya Tanzania.Pia nasoma vitabu tofauti tofauti vyenye kuchochea mtazamo a chanya.
Mazoea haya huniwezesha “kujua ukweli wa mambo” unaoendelea katika jamii na maisha kwa ujumla, pia kuandika makala mbali mbali ndani ya Jielimishe Kwanza!… hii ikiwa ni dhana kubwa ya Jielimishe Kwanza!
Hii haina madhara yoyote katika masuala yangu ya shule...najua! wenzangu na mimi wanaosomea shahada ya Uzamili-"Master's" hujikita zaidi kwenye kusoma mambo yanayoendana na masomo ya darasani tu! Nashauri, Wakati mwingine ni vizuri kusoma mambo yahusuyo jamii moja kwa moja na maisha kwa ujumla wake.
Leo, Jumapili, Mei, 18 2014 saa 24:0 AM nimekutana na gazeti la Tanzania liitwalo Mwananchi lenye kauli mbiu "Fikiri Tofauti" ...hakika kuna makala napenda nikushirikishe kuhusu suala zima la msomi wa Chuo kikuu kupenda/kutegemea/kutarajia kuajiriwa.
Mwandishi, Herieth Makwetta, wa gazeti hilo Kanihamasisha! Kukuhamasisha! kubadili mtazamo, hasa alipoandika makala kutokana na mahojiano ya msanii wa Hip Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon almaarufu kama "Nikki wa II" mwenye shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDMS).
Ama kwa hakika, "Nikki wa II" ni mfano wa kuigwa kwa vijana wasomi wenye shahada nchini Tanzania. Ukiwa msomi wa Sekondari au chuo kikuu nakushauri sikiliza kwa makini wimbo wake mpya ujulikanao kwa jina la “Sitaki Kazi” utakubaliana nami.
Naomba ufanyie kazi sehemu ya mashairi ndani ya wimbo wake, anasema;
"Sitafuti kazi ila nataka nitafutwe na watu wanaotafuta kazi"
Pia, anasisitiza kutokuwa mtumwa wa kazi sanjali na moja ya makala zetu kama; athari za kufanya kazi katika mazingira ya utumwa wa kisasa na kufanya kazi unayoipenda.
Naomba nisiendelee kuandika zaidi, ili uweze kupata muda wa kusoma kwa haraka na kutafakari yaliyomo ndani ya wimbo huo.Nakutakia utendaji kazi mwema, najua tena siku ya Jumatatu!
Imetayarishwa na kutolewa na
Jielimishe Kwanza!